BONNAH AWATETEA WASTAAFU BUNGENI


Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

MBUNGE wa Segerea Bonnah Kamoli ameuliza je, lini kanuni mpya za malipo ya Pensheni kwa Wastaafu ya kila mwezi ya kutoka asilimia 50 mpaka 67 itaanza kutumika? katika swali lake la msingi.

Akijibu swali hilo bungeni leo bungeni  Februari 5,2024 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi alisema kuwa Serikali kupitia Gazette la Serikali Namba 357 la Mei 20, 2022 ilitangaza Kanuni Mpya ya Mafao ambayo iliboresha kiwango cha mafao ya pensheni ya kila mwezi kwa wastaafu kutoka asilimia 50 iliyokuwa ikilipwa awali na kuwa asilimia 67 kwamba na Matumizi ya Kanuni hizo yalianza kutumika rasmi Julai 1, 2022. 

Naibu Waziri huyo ameeleza kanuni hizo ziliandaliwa kwa kushirikisha wadau wote (Serikali, Wafanyakazi na Waajiri) kwa lengo la kufanya maboresho ya Pensheni ili kuwianisha mafao ya wanachama na kuifanya Mifuko kuwa endelevu.

Aidha katika swali la ngongeza Bonnah amesema kuwa pamoja na majibu mazuri ya serikali bado baadhi ya wastaafu hao wanalalamika hawapati mafao yao na kwamba waliopo Zanzibar tayari wameshaongezewa kulingana na viwango vyao Je serikali ya Tanzania Bara ina mipango gani ili nao wastaafu waweze kuongezewa?

Naibu Waziri Katambi akijibu swali hilo la ngongeza amesema kuwa ni lazima wakiri na wawe wazi kwa kazi kubwa aliyoifanya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kupitia ofisi ya Waziri Mkuu.

" Tulikuwa na changamoto kubwa awali na tunakiri mifuko kuwa mingi lakini tulijaribu kuoanisha itasababisha kwenda kuitumia mifumo mpya wa kikokotoo ambapo kwa sasa mkupuo wa mafao tunalipa asilimia 50 hadi 67 na ile pensheni ya kila siku inatoka ndani ya siku 30 " amesema Naibu Waziri Katambi.

Amefafanua kuwa suala la Zanzibar sio la kimuungano wenzao wametangulia huku akiwapongeza na kusema nao tayari wapo kwenye hatua nzuri ya kuleta tathimini taarifa ambayo itaangalia ustamilivu wa mifuko na kiwango cha upatikanaji wa mafao kama kimepanda.

Naibu Waziri Katambi ameongeza kuwa wanaenda kufanya maboresho hayo na litakuwa ni zoezi la haraka la miaka mitatu ya kufanya tathimini na imeshatimia na kwamba wapo kwenye zoezi hilo.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI