MBUNGE AISHAURI SERIKALI KUBORESHA KANUNI ZA UHIFADHI

Na Asha Mwakyonde Dodoma

MBUNGE wa Nkasi Kaskazini Aida Kenani (CHADEMA), ameshauri Mamlaka za Serikali ziwasiliane pindi vijiji vinapoanzishwa lengo likiwa ni kujua mapema kama eneo ni sahihi kwa ajili ya makazi ya watu na shughuli nyingine za kibinadamu ili kuondoa sintofahamu baina ya wananchi na hifadhi nchini.

Pia ameishauri Serikali kuboresha kanuni za uhifadhi ambazo zimepitwa na wakati na kusababisha wananchi kuendelea kuwa masikini kutokana na kulipwa fidia kidogo pindi mazao yao yanapoliwa na wanyama wanaotoka hifadhini.

Hayo  ameyasema  Februari 8,2024 wakati akichangia utekelezaji wa shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Ardhi, Maliasili na Utalii kwa mwaka 2023 ameeleza lengo ni kufanya uhifadhi wa kisasa wenye tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla kwa kuondoa migogoro ya ardhi baina ya wanachi na hifadhi.

Amesema wananchi wamekuwa wakitozwa faini za mamilioni ya shilingi pindi inapotokea amemjeruhi ama amemuua mnyama mkali wakati akitetea ili asimdhuru.

Kenani  ameeleza kuwa kanuni amesema kanuni za mwaka 2011   zinaleta doa kwenye Taifa na  sifa mbaya kutokana na kuthamini Wanyama kuliko binadamu.

Mbunge huyo ametolea mfano katika eneo la kifuta machozi kwa binadamu  ambapo mwananchi akipata madhara kutokana na wanyama wakali na waharibifu, akijeruhiwa anatakiwa kulipwa kifuta machozi shilingi laki mbili, mkono au mguu ikikatika kabisa analipwa tena na akifariki  kifuta machozi ni shilongi milioni 1.

 “ Taifa linaangalia thamani ya mwanadamu sawa na shilingi milioni 1? hii halikubaliki, tumefanya mabadiliko ya vitu vingi  kuna shida gani kwenye kanuni hizi? ," amehoji Kenani.

Aidha ameeleza kuwa ni vyema Serikali ikawa mfano kama inavyotaka wananchi wafuge kisasa kwenye eneo dogo, yenyewe iwe mfano hali itakayosaidia kupunguza ama kuondoa kabisa migogoro ya ardhi baina ya wananchi na hifadhi

Akichangia upande wa mazao ameeleza kuwa nako kuna changamoto  wanyama wakali na waharibifu huku akisema mwananchi ambaye amelima mita 500 kutoka eneo la hifadhi ,wanyama wakila heka moja analipwa sh.25,000 ambapo  mfuko mmoja wa mbolea unauzwa hadi sh 70,000, ekari moja ambayo angevuna zaidi ya gunia 25 ,na maandalizi yake hadi anavuna ni takribani sh.750,000 halafu Serikali inasema itamlipa 25000.

Amesema kutoka kilomita moja hadi  kilomita nne eneo la hifadhi kama wanyama wamekula mazao ya mwananchi analipwa sh.75000 au 100,000.

“Serikali ituambie ni wapi ataenda kununua gunia 25 kwa sh.25000,kanuni zinawapa umasikini watanzania,ukitoka kuanzia mita 501 mpaka kilomita moja anatakiwa alipwe sh.50,000 kwa ekari hizi kanuni zifanyiwe marekebisho," ameeleza.

Mbunge huyo ameongeza kuwa 
kanuni hizo waziri ana Mamlaka nazo  huku alihoji kwa nini wanazungumza kila siku ,zinaleta sura mbaya nchini ni jambo ambalo halipendezi  na kwamba ,inawezekana kanuni zilikuwa zinatumika  kipindi hicho kwa sasa zimepitwa na wakati.

"Mwanadamu anapopambana na h
mnyama mkali akimuua tu anatakiwa kulipa shilingi milioni 30, kwa nini thamani ya mnyama iwe kubwa kuliko ya binadamu ni aibu kuendelea kujadili kanuni kama hizi ndani ya bunge hili," amesema.

Amesema wanategemea serikali inakwenda kulichukua hili jambo kwa umuhimu mkubwa najua hata Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA),
kuna wakati wanasema sisi hatuwezi kuvuna hawa tembo ,badala yake wanawasukuma hifadhini.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI