DCEA: MADHARA YA KULIMA BANGI NA MIRUNGI HUONDOA UOTO WA ASILI

Na Asha Mwakyonde Dodoma 

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),miongoni mwa madhara makubwa yanayopatikana kwa kulima bhangi na mirungi ni kusababisha kuondoa uoto wa asili.

Hayo yameelezwa leo Agosti 04,2024 na Afisa Elimu kutoka mamlaka hiyo,Said Madadi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya Kitaifa ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma amesema inapolimwa bangi, mirungi ile miti au mazao mengine hayalimwi maeneo hayo.

Amesema wanaolima bangi, mirungi wanafanya kama mazao mbadala ya chakula na kwamba hatari yake ni njaa baadae.

Afisa huyo ametolea mfano maeneo ambayo bangi hulimwa hakuna miti mikubwa inayotumika kama sehemu ya utunzaji wa Mazingira.

Amesema lengo la kuwepo kwenye maonesho hayo ni utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo ya kutoa elimu kwa makundi mbalimbali kuhusiana na madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na wakulima kuacha kujihusisha na Kilimo hicho.

"Athari kubwa ya matumizi ya mirungi ni kusababisha saratani, pamoja na upungufu wa nguvu za kiume,"ameeleza Afisa elimu huyo.

Naye Mfamasia Mwandamizi kutoka DCEA, Upendo Chenya ameeleza kuwa wanatoa tiba kwa watumiaji, waraghibu kwa kushirikiana na Wizara ya afya lengo likiwa ni kupunguza madhara yatokanayo na bangi na mirungi.

Mfamasia huyo ameongeza kuwa serikali imekuwa ikiboresha huduma za tiba katika vituo vya afya katika kila kituo cha afya, Hospitali ambapo kuna kitengo cha afya ya akili ambapo vituo zaidi ya 16 nchini na vimeweza kusajili.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA