TMDA: NYARAKA ZOTE ZENYE USAJILI ZINAPIMWA, WANANCHI WAKARIBISHWA KUTEMBELEA BANDA LAO NANE NANE DODOMA


Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), inahakikisha nyaraka zote zenye usajili na bidhaa zinapimwa ili kujua kama zimezingatia vigezo na kuhakikisha bidhaa hizo zinazoingia kwenye soko zikiwa na ubora ,usalama na ufanisi unaotakiwa.

Pia wananchi wameshauriwa kutembelea banda la mamlaka hiyo katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) ili kuweza kujifunza masuala mbalimbali yakiwamo matumizi sahihi ya dawa.

Akizungumza leo Agosti 4,2024 katika maonesho hayo yanayofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya nane nane Nzuguni Meneja kutoka TMDA Kanda ya Kati, Sonia Mkumbwa ameeleza kuwa ili waweze kuhakikisha usalama na ufanisi huo unatimilika, kuna majukumu ambayo mamlaka inayafanya.

Meneja huyo amesema kuwa mamalaka hiyo ina jukumu la kuhakikisha bidhaa zote zinazoingia nchini zimesajiliwa na hata zile zinazozalishwa katika viwanda vya ndani.

"Tunadhibiti ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za dawa, vifaatiba na vitendanishi ili bidhaa hizi zinapoenda kutumika kwa wananchi hasa wagonjwa ziwe salama lakini pia wananchi waache matumizi ya dawa kiholela,"amesema Meneja huyo.

Akizungumzia ushiriki wao katika maonesho hayo amesema ni kutoa elimu hususani ya matumizi sahihi ya dawa, namna ya kutupata na kwamba ikiwa magonjwa ana malalamiko wanayapokea ili waweze kufanya huduma bora zaidi kwa Watanzania waweze kuwa na afya njema.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA