Na Asha Mwakyonde,Dodoma
MWANAFUNZI wa Chuo Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), fani ya Uhandisi wa Mitambo (Mechanical Engineering), Samwel Oscar amebuni mashine ya kusambaza mbolea shambani kwa kutumia umeme wa JUA kwa lengo la kunrahisishia mkulima na kumpunguzia muda katika kazi ya Usambazaji wa mbalea hiyo.
Akizungumza katika maonesho ya wakulima na Wafugaji Nane nane ambayo yanafanyika Kitaifa viwanja vya nane nane Nzuguni jijini Dodoma kwenye banda la chuo hicho amesema kuwa ameona changamoto ambazo wanazipitia wakulima wakati wa kusambaza mbolea shambani ambao wanatumia mikono hali inayowasababishia kupoteza muda mwingi kwenye usambazaji wa mbolea hiyo.
Mwanafunzi huyo ameeleza kuwa kupitia mashine hiyo mkulima anaweza kutumia muda mchache kukamilisha zoezi la usambazaji wa mbalea.
"Mashine hii ina uwezo wa kusambaza mbolea katika shamba la ekari moja hadi tatu kutegemeana na ukubwa wa shamba," amesema Oscar.
Kwa upande wake Ofisa Uhusiano Mkuu wa NIT, Tulizo Chusi, amesema wapo katika maonesho hayo ile kuonesha bunifu mbalimbali wanafunzi wao lengo likiwa ni kuwahawasisha vijana kujiunga chuo hicho.
0 Comments