TCAA: WAENDESHA DRONES LAZIMA WAWE NA VIBALI, YASHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE DODOMA KUTOA ELIMU


Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari ameeleza kuwa uendeshaji wa matumizi ya ndege nyuki maarufu (DRONES), ni lazima waendeshaji wahudhurie mafunzo badala ya kutumia vifaa hivyo kiholela.

Hayo ameyasema leo Agosti 5, 2024 kwenye banda lao la TCAA lililopo katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma amesema wanaotumia ndege nyuki wanapaswa kupata vibali vya kuendesha chombo hicho, leseni stahiki.

Ameongeza kuwa anayeendesha chombo hicho ni kama rubani lazima apate mafunzo stahiki kwa lengo la kujua kanuni za kianga ili aweze kuitumia ndege nyuki.

Mkurugenzi huyo amesema wanaendesha mradi wa Chuo cha Usafiri wa Anga ambacho kinafundisha mafunzo ya Anga na kwamba kina dahili wanafunzi wa Kitaifa na kimataifa.

Ameongeza kuwa tayari wameshapata fedha kutoka serikalini kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Chuo hicho cha Usafiri wa Anga huku akisema serikali imeshawapatia ardhi na kwamba michoro imekamilika ambapo gharama yake ni kiasi cha Sh. Bilioni 78.


Naye Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC), Aristid Kanje ameeleza kuwa wanaenda na Teknolojia ambapo mtu  akitumia drones kwaajili ya kufanya ukaguzi wa shamba lake kujua sehemu ya kuweka dawa, mbolea ndege nyuki itamfanya aweza kuona kilimo chake kumekuwa rahisi.

Akizungumzia maonesho hayo  ameeleza kuwa wapo kwa ajili ya kuwaeleza wananchi fursa zilizopo katika usafiri wa anga ili wawapeleke vijana kupata mafunzo ambapo wanaweza kupata ajira ndani ya taifa na nje  kwa kuwa Sekta ya Anga ni chachu kwa maendeleo katika kila nyanja.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA