FCC YAWAKUMBUSHA WAFANYABIASHARA KUZINGATIA UBORA WA BIDHAA

Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), William Erio amesema kuwa wafanyabiashara wanapaswa kuhakikisha bidhaa zao zinakidhi viwango vya ubora na vinavyotambulika vya kisheria.

Pia amewataka Wafanyabiashara na wakulima kujitokeza katika kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga kura lengo likiwa ni kupata nafasi ya kuwachagua Viongozi wenye sifa.

Hayo amesema leo Agosti 5, 2024 kwenye Maonesho ya wakulima na Wafugaji yanayofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma amesema kuwa FCC wanajukumu la kuhakikisha mfanyabiashara anatambua wajibu wake katika soko ili kuboresha bidhaa ambazo zitakuwa na tija.

"Mfanyabiashara anapaswa kujitofautisha kupitia bidhaa zake katika soko la ushindani na hii itamsaidia itaboresha ubora, kuongeza vipengele vya kipekee katika kutoahuduma bora," ameeleza.

Akizungumzia daftari la mpiga kura amesema viongozi bora na wenye sifa ndio watakao kuwa na mipango thabiti na mikakati ya maendeleo ya kilimo na kuweza kujumuisha mipango ya kuboresha miundombinu, masoko, na upatikanaji wa huduma za kilimo.

Kuhusu maonesho amesema wana umuhimu wa kushiriki kwa lengo la kutoa elimu kwa wafanyabiashara, wakulima huku akiwataka kutembelea banda lao FCC ambayo itawasaidia katika biashara zao.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA