MWANAFUNZI NIT ABUNI TEKNOLOJIA YA KUKUZIA VIFARANGA VYA KUKU

Na Asha Mwakyonde Dodoma 

KUTOKANA ukuaji wa teknolojia katka nyanja mbalimbali ikiwamo ya kilimo mwanafunzi wa mwaka wa nne katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), fani ya Uhandisi wa Mitambo, George Luambano, amebuni mashine kukuzia vifaranga vya kuku.

Mashine hiyo ambayo inatumia taa za joto na endapo joto hilo likipungua zinaendelea kuwaka na kwamba inayosaidia kulea vifaranga kwa kutumia teknolojia lengo ubunifu huo ni kumrahisishia mfugaji wa kuku na kiepukana na adha ya kwenda kuwahudumia mara kwa mara.

Hayo ameyasema leo Agosti 5,2024 katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma amesema kuwa lengo la kubuni ameeleza kuwa ameongeza mashine hiyo ili kuhakikisha kila mfugaji anaweza kukuza vifaranga na kupunguza vifo vya vifaranga hivyo.

Pia amesema kuwa Mashine hiyo inasaidia kulisha kuku, kuwapa maji kwa muda maalumu, kuwapa joto na unyevunyevu huku akisema inampunguzia mfugaji majukumu.

Amesema kuwa katika mashine hiyo mfugaji atawawekea vifaranga maji na chakula ambapo vikiisha inatoa taarifa kwa kupiga kelele kuashiria maji, chakula kimoja wapo kimeisha au viamepungua.

"Joto linalohitajika kwa kuku (nyuzi 33) taa zitazima na kuku ataendelea kukua na kwamba ina feni ambayo inaingiza hewa ndani," ameeleza Luambano.

Naye Ofisa Uhusiano Mkuu wa NIT, Tulizo Chusi, amesema kuna bunifu zimesajiliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) kwa ajili ya kwenda kwa walaji.ambazo zinatoka katika kampuni kutoka katika Chuo hicho ambayo inafanya kazi ya kuendeleza bunifu za vijana hao na kuziingiza sokoni.

Post a Comment

0 Comments

 MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI