TARURA: UBOVU WA BARABARA UNASABABISHWA KUTOKUPIMA UDONGO

Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), umesema kuwa barabara inaanzia maabara ili itengenezwe barabara hiyo lazima ianze maabara kwa kupima sampuli za udongo, Kokoto au lami.

Hayo yamesemwa leo Agosti 05, 2024, katika maonesho ya wakulima na Wafugaji (Nane nane) ambayo yanafanyika Kitaifa viwanja vya ane nane Nzuguni jijini Dodoma na Fundi Sanifu Mkuu Maabara ya Wakala wa Barabara za VTARURA, Jacob Manguye 

amesema kuwa barabara nyingi zinafeli ,kushindwa kuwa za kiwango kutokana na watu wengi kutokupima kupima udongo kabla ya kuanza ujenzi.

Amesema kuwa TARURA ina maabara ambayo ya kupima udongo ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kusimamia kazi, ubora wa barabara za kutoka vijijini hadi na mijini ambazo zinateketezwa katika miradi mbalimbali hapa nchini.

Fundi Sanifu huyo ameeleza kuwa kazi ya maabara hiyo ni kuthibitisha ubora na kupitia maabara ya udongo wanatarajia kuwa na kazi nzuri za kiwango zunazotakiwa ili kuondokana na kashfa za kazi kuwa chini ya kiwango.

"Kwa sasa barabara za TARURA zina ubora wa viwango vinavyotakiwa na tunajihidi kupanua barabara hizo zipitike vijijini,"ameeleza.

Akizungumza maonesho hayo amesema kuwa Wakala huo umeshiriki kwa kuwa wana uhusiano na wakulima na Wafugaji hutumia barabara kusafirisha mazao yao kupitia barabara zinazojengwa na TARURA.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU