CHATANDA AFANIKISHA UKAMILISHAJI WA UJENZI WA NYUMBA YA MJANE IRINGA

Iringa 

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda (MCC) katika Ziara yake ya Kikazi amekagua maendeleo ya Ujenzi wa Nyumba ya mjane Mama Maria Ngoda,ambaye alikuwa amebambikiwa Kesi ya Uwindaji haramu baada ya kukutwa na vipande vya Swala, UWT ikiongozwa na Mwenyekiti wake  Chatanda (MCC) pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Ndg. Zainab Khamis Shomari (MNEC) ilisimama kumtetea na kuhakikisha haki inatendeka na kuwa huru.

Aidha,UWT awali ilitoa kiasi cha shilingi Milioni tano (5) Kwa lengo la kumpa kitega Uchumi, hata hivyo UWT Mkoa wakishirikiana na mlemgwa waliamua kumtafutia Kiwanja na kuanzisha Ujenzi wa Nyumba ya makazi. Ambaayo imetembelewa na kukaguliwa na kufanyika harambee Kwa lengo la kukamilisha Ujenzi Ili Nyumba iweze kutumika mwisho wa mwezi Januari 2025.

Wachangiaji,Wabunge wa Viti Maalumu, Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT, Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji Mkoa, Wanachama wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wamemuunga Mkono MCC Chatanda Kwa michango ya Fedha, Vifaa kama Cimenti, Mbao, Mabati, Vigae Vyenye Jumla ya thamani ya shilingi Milioni 10.

Chatanda amewataka Wanawake wote Nchini kuwa na Moyo wa Upendo, Ushirikiano kama wanadamu Kila mmoja anazo nyakati ngumu kama jambo la Maria Ngoda lilivyogusa mioyo ya Watanzania lakini Wanawake wameonesha Upendo na Mshikamano wao Kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kumtetea na kumsaidia.

Hongereni sana Wanawake wa Tanzania.

#uwtimara

#wanawakejeshikubwa

#kaziiendelee





 

Post a Comment

0 Comments

WAUGUZI, WAKUNGA ENDELENI KUBEBA DHAMANA KAMA SERIKALI ILIVYOWEKEZA