KATIMBA: KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA KUANZA DODOMA APRILI 30 MWAKA HUU

📍Serikali kuanza awamu ya pili ya msaada wa kisheria nchi nzima

Na Mwandishi wetu, DODOMA 

NAIBU Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Zainab Katimba, amesema kuwa, Wizara inatarajia kuanza rasmi utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia awamu ya pili (Mama Samia Legal Aid Campaign Phase II).

Katimba ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma Aprili 24, 2026, na kufafanua kuwa utekelezaji wa Kampeni hiyo itaanza rasmi Aprili 30 mwaka huu ambapo huduma za Msaada wa Kisheria zitatolewa kwa muda wa siku 15 katika Halmashauri zote na Kata zote za Mkoa wa Dodoma na hatimaye kuifikia mikoa yote nchini.

Post a Comment

0 Comments

TANZANIA YAENDELEA KUJIIMARISHA KATIKA USIMAMIZI WA MAAFA