Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KUTHAMINI mchango wa viongozi waliolitumikia Taifa katika kulijenga na kuliendeleza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ni miongoni mwa hatua zinazolenga kudumisha uhusiano na kuhifadhi uzoefu wa uongozi wa kijeshi, huku Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dkt. Rhimo Nyansaho, akiwatembelea Wakuu wa Majeshi Wastaafu, Jenerali Robert Mboma na Jenerali Davies Mwamunyange.
Katika ziara hiyo iliyofanyika Oktoba 27, 2026, jijini Dar es Salaam, Dkt. Nyansaho aliwatembelea viongozi hao katika makazi yao yaliyopo Mbweni na Tangi Bovu, kwa lengo la kuwajulia hali na kufanya mazungumzo nao.
Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa juhudi za Waziri huyo kuwatembelea na kuwasiliana na viongozi waandamizi wastaafu wa JWTZ, kama ishara ya kuthamini mchango wao katika kulitumikia Taifa na kulijenga jeshi hilo.
Kupitia mazungumzo na viongozi hao, Dkt. Nyansaho anaendelea kudumisha uhusiano na viongozi wenye uzoefu na historia muhimu katika uongozi na maendeleo ya JWTZ.
Hatua hiyo pia inaonesha umuhimu wa kutambua mchango wa viongozi wastaafu katika taasisi za ulinzi wa Taifa na kuendeleza mawasiliano kati yao na uongozi uliopo madarakani.







0 Comments