Na Asha Mwakyonde
SALOME Zabron, mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam, anahitaji msaada wa Watanzania wenye moyo wa kujitolea ili aweze kuendelea na masomo ya chuo kikuu baada ya kufaulu kidato cha tano na sita, lakini kukosa mkopo wa elimu ya juu.
Salome, ambaye ni yatima, amepitia changamoto nyingi za maisha tangu akiwa mdogo. Mama yake alifariki dunia akiwa na umri wa miaka mitano, huku baba yake akifariki alipokuwa akisoma kidato cha pili.
Licha ya kukabiliwa na misukosuko hiyo, Salome hakukata tamaa ya kusoma. Alijitahidi kuendelea na masomo hadi alipofaulu kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Jokate Mwegeleo, hatua inayomfungulia fursa ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu.
Hata hivyo, ndoto yake ya kuendelea na masomo inakabiliwa na changamoto ya kifedha baada ya kukosa mkopo wa elimu ya juu, hali inayohitaji moyo wa huruma na mshikamano kutoka kwa jamii.
Kutokana na hali hiyo, Watanzania, taasisi, wadau wa elimu na watu binafsi kuungana kumsaidia Salome kwa kadiri iwezekanavyo kupitia Namba ya simu ya Kiganjiani, Mtandao wa Airtel 0784 157 721 Salome Zabron,ili apate nafasi ya kuendelea na masomo na kujenga maisha bora ya baadaye.
Msaada wowote, iwe ni fedha au mahitaji mengine ya kielimu, unaweza kuwa hatua muhimu katika kumsaidia Salome kufikia ndoto yake ya kupata elimu ya chuo kikuu.
Tushirikiane kumsaidia Salome. Kila mchango una thamani na unaweza kuwa sababu ya kuendeleza safari yake ya elimu.
Mungu awabariki wote watakaoguswa na hali yake na kujitokeza kumsaidia.

0 Comments