MMOJA wa washiri wa kongamano hilo hilo kutoka Arusha ambaye pia ni Mkurugenzi mmiliki wa kampuni ya ulinzi ya Security Tanzania Co.LTD (ADF), Frank Akya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano.
Na Asha Mwakyonde,Dodoma
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini amesema kazi zinazofanywa na kampuni binafisi za ulinzi zinasaidia Jeshi la Polisi nchini katika majukumu yake.
Pia Waziri Sagini amewataka Wakurungenzi wamiliki wa kampuni binafisi za ulinzi Tanzania Bara na Zanzibar kushirikiana pamoja na kuwa na Umoja ili waweze kufika mbali katika kuyafikia majengo yao.
Waziri Sagini ameyasema hayo Aprili 8,2022 jijini hapa wakati akizungumza na Wakurungenzi Wamiliki wa kampuni binafisi za ulinzi Tanzania Bara na Zanzibar katika kongamano la kujadili masuala mbalimbali yakiwamo changamoto na mafanikio, amesema kampuni hizo zinafanya kazi njema ya kusaidia ulinzi na usalama wa wananchi.
Amesema hali hiyo imeimarisha ukuaji wa uchumi na hata wawekezaji wamekuja kuwekeza nchini na kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania na kwamba Jeshi Polisi limekuwa likishirikiana na kampuni hizo.
"Kuwa kucheleweshwa kwa mishahara kunachangia kwa baadhi watumishi wanaofanya kazi katika kampuni binafisi za ulinzi kupata tamaa ya kufanya vitendo vya kiualifu," amesema Naibu Waziri Sagini.
Sagini amewataka Wakurungenzi wamiliki hao kuanzisha mfumo wa Kanzi Data itakayowasiadia kujua watu wanaowajiri.
Naye Katibu Mkuu wa kongamano hilo Comradi Manyama amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kukutana na kujadili changamoto za kiutendaji ambapo zaidi ya kampuni 130 zimekutana.
Amesema hiyo inaweza kuwapatia uzoefu wa kiutendaji na kwamba wanachangamoto nyinyi za wataja wao wanaowafanyia kazi kwa upande wa malipo.
"Tunatoa huduma kwa wateja wetu lakini namna ya ulipaji imekuwa ni changamoto kwani wamekuwa wajichelewesha malipo na hii inakuwa ni changamoto pia kwa wanaotufanyia kazi pale wanapo hitaji mishahara yao kwa ajili ya kujikimu na familia zao," amesema Manyama.
Manyama ametoa wito kwa wateja wao kuwa watambue kazi wanazizifanya ni kwa ajili ya usalama wao na mali zao hivyo walipe mapema ili wawalipe wanaofanya nao kazi walipwe kwa wakati.
Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo kutoka Arusha ambaye pia ni mkurugenzi mmiliki wa kampuni ya ulinzi ya Security Tanzania Co. LTD ( ADF),Frank Akya amesema kuwa tangu miaka zaidi ya 40 hawajawahi kukutana wadau wa ulinzi katika kongamano hilo wanejifunza mengi.
" Namshukuru Naibu Waziri Sagini anetufungua masikio kwa yale ambayo hatukuwa na uelewa nayo katika masula ya ulinzi ameongea machache lakini ameeleweka. Kwa kweli sijapoteza muda nimejifunza vitu vingi yakimo ya utunzaji wa silaha," amesema.
Aidha amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa amekuwa ni mama anayehitaji ushirikiano ili waweze kujenga ulinzi imara na usalama.
" Natamani hii amani tuliyonayo tuendelee kuitunza kama mama yetu Samia anavyotaka nasi kupitia ushirikiano wa kampuni zetu tutaendelea kuitunza amani yetu isipotee," ameeleza Akya.
Pia amewataka Wakurungenzi wamiliki wa kampuni hizo kutunza silaha zao vizuri na kuajiri vijana ambao watanashati 'Smart' na wenyewe maadili mewma.
0 Comments