OSHA: IDADI YA MAENEO YA KAZI YALIYOSAJILIWA YAONGEZEKA

 

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

WAKALA wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA),umesema kuwa  umejipanga kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kisasa vya ukaguzi ambavyo  vinavyoendana na mabadiliko ya teknolojia ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu muhimu ya kutolea huduma za Usalama na afya.

OSHA ni Wakala wa Serikali ambao upo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu ulianzishwa tarehe 31 Agosti 2001 chini ya Sheria ya Wakala za Serikali Na 30 ya mwaka 1997 kama sehemu ya maboresho katika utoaji wa huduma za Serikali kwa wananchi.

Akizungumza Machi 4,2023 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji na mafanikio ya OSHA katika kusimamia Sheria ya Usalama na Afya mahala pa kazi kwa kipindi cha miaka miwili ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ,Mkurugenzi Mkuu wa Wakala huo Hadija Mwenda amesema miundombinu mingine itakayojengwa ni pamoja na maabara za kisasa za uchunguzi wa sampuli mbalimbali zinazochukuliwa katika sehemu za Kazi

Mkurugenzi huyo ameeleza  kuwa Wakala huo  umefanikiwa kuongeza idadi ya maeneo ya Kazi yaliyosajiliwa kutoka 4,336 hadi 11,957 ongezeko hilo ni sawa na asilimia 276

"Idadi ya kaguzi zilizofanyika zimeongezeka kutoka kaguzi 104,203 hadi kufikia kaguzi 322,241 sawa na asilimia 132," amesema Mkurugenzi huyo.

Ameongeza kuwa Wakala huo unatarajia kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na umuhimu wa kufanya shughuli mbalimbali kwa kuzingatia kanuni bora za Usalama na Afya Mahala pa Kazi pamoja na kuendesha majadiliano na wadau juu ya utekelezaji wa Sheria ya Afya na Usalama Mahala pa Kazi kupitia semina, mikutano,makongamano na maonesho mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI