SELF MF YATOA MIKOPO KWA WANUFAIKA 225,000 NCHINI


Na Asha Mwakyonde, Dodoma

ZAIDI wajasiriamali,vikundi 225,000 wamenufaika na  Mfuko wa Self Microfinance Fund tangu kuanzishwa kwa mfuko huo ambapo kiasi cha shilingi bilioni 313 kimetolewa.

Pia Mfuko wa Self umejipanga kuhakikisha Asasi zenye kutoa Mikopo zinajengewa uwezo mkubwa wa kuhudumia wakulima na Wajasiriamali wenye uhitaji wa kifedha katika shughuli za kilimo.

Akizungumza Jijini Dodoma Machi 01,2023, katika Warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo Waandishi wa habari, Meneja Masoko na Uhamasishaji wajasiriamali  kutoka mfuko huo Linda Mshana amesema lengo la mfuko huo ni kufungua matawi kila mkoa ili kuwahudumia wajasiriamali mmoja mmoja pamoja na vikundi ambavyo vipo katika mikoa husika.

Linda ameeleza kuwa urejeshaji wa mikopo ni asilimia 93 hali iliyosababisha mtaji kukua kutoka bilioni 62 hadi kufika zaidi ya bilioni 300, tangu kuanzishwa kwa Self Microfinance Fund.

Amesema dhumuni la Self Microfinance Fund ni kuhakikisha Asasi hizo zinatoa Mikopo  kuwawezesha wakulima kukidhi mahitaji ya kifedha ili kurahisisha upatikanaji wa vifaa vya kilimo na pembejeo kwa wakulima na wafugaji.

"Huduma za Mfuko wa Self inalengo la kukuza na kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa Wananchi hususani wa Vijijini, na hivyo kuwapa fursa ya kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali kwa lengo la kujiongezea kipato ili kuondokana na umaskini," amesema Linda.

Ameongeza wapo katika kuwahudumia wakulima kwenye shughuli za pembejeo, uvunaji, uuzaji wa mazao ikiwa ni pamoja na shughuli za Mfumo wa stakabadhi mazao ghalani.


Akizungumzia changamoto katika urejeshaji wa mikopo Meneja wa Tawi  la Dodoma Aristid Tesha  amesema kuwa mkopaji anaweza kushindwa kurejesha kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo kufilisika, changamoto za kiafya na kwamba katika huduma za kifedha changamoto hizo hazikwepeki.

"Changamoto hizi huwa tunaziangalia kwa mapana yake, kwa dunia ya sasa mikopo inakuwa na bima isipokuwa mikopo ambayo tunazikopesha kampuni kwa kuwa kamapuni ilivyo ni kama mfanyabiashara wengine kuna ugumu kuweka bima lakini mikopo mingine inakuwa na bima," amesema.

Amefafanua kuwa bima iliyotolewa na Self Microfinance Fund ni asilimia 0. 6 kwa mwaka huku akitolea mfano mteja anayechukua milioni 10 kwa mwaka mmoja ni asilimia 60.

Hata hivyo mara baada ya warsha hiyo waandishi wa habari waliwatembelea baadhi ya wanufaika wa mikopo ya Self Microfinance Fund, Aziza Abdullah na Wema Sehaba.


Mfanyabiashara wa kuchakata makopo ya maji yaliyotumika  Aziza Abdallah ameushukuru Mfuko huo kwa kumuamini na kumkopesha  shilingi milioni 50 ambapo zimemsaidia kukuza biashara yake.

"Nawashauri wanawake wenzangu wasikate tamaa katika kila wanachokifanya wakikiamini watafanikiwa mimi nilikuwa naokota makopo jamii ilinichukulia kuwa nimepata kichaa cha ujauzito kwa kuwa nilikuwa mjamzito lakini sikukata tamaa hadi hapa nilipofikia," amesema Aziza.


Naye Wema Sehaba mfanyabiashara ambaye ni mnufaika mfuko huo WEMA AGROVET  anaye anajishughilisha na uuzaji pembejeo za kilimo amesema kuwa amefanikiwa kukopa milioni 40 katika mfuko wa SELF na zimemsaidia katika kukuza biashara yake ikiwemo kufungua matawi mengine ya biashara yake hadi vijijini.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU