ASILIMIA 80 YA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA TANZTECH NI WANAWAKE


 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TANZTECH ELECTRONICS LIMITED, Gurveer Hans alipotembelea banda la Kampuni hiyo. 

Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya 
TANZTECH ELECTRONICS LIMITED iliyopo Jijini Arusha, Gurveer Hans amesema kuwa hivi karibuni wnatarajia kuanza kuuza na kusambaza bidhaa wanazozalisha endapo watakamilisha tarabibu zote zinazotakiwa kisheria.

Akizungumza jijini Dodoma Aprili 25,2023 kwenye banda la Kampuni hiyo katika maonesho ya wiki ya Ubunifu Kitaifa (IWTZ),yenye kauli mbinu isemayo ' Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kuchangia Uchumi wa Bluu', wakati akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule alipotembelea banda hilo, Hans ameeleza kuwa Kampuni hiyo inajihusisha na utengenezaji wa kompyuta mpakato, simu za mkononi ,Tablets, projekta  na vifaa vingine ambavyo vinatumia umeme.

Mkurugenzi huyo amesema lengo la kuwepo katika maonesho hayo ni kumtambulisha bidhaa zao ambazo wanatarajia kuziweka sokoni hivi karibuni.

Ameongeza kuwa asilimia 90 ya wafanyazi wao ni wahitimu wa Vyuo Vikuu vya hapa nchini na kwamba asilimia 80 ni wanawake.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary ameipongeza Kampuni hiyo kwani imeendana na agenda ya Tanzania huku akiwakaribisha kuweka tawi lao mkoani hapa.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU