Na Asha Mwakyonde,Dodoma
TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), imesema kuwa ina kozi za muda mrefu na mfupi ambazo ni fursa kwa vijana ambapo baada ya miezi miwili wanaweza kujiajiri na kuajiriwa kwa lengo la kukabiliana na changamoto za ajira.
Akizungumza Jijini Dodoma Aprili 26,2023 kwenye maonesho ya wiki ya Ubunifu Kitaifa (IWTZ),yenye kauli mbiu isemayo 'Ubunifu kuchangia uchumi Shindani,' ambayo yanaendelea katika viwanja vya Jamuhuri, Mwalimu wa DIT campus ya Mwanza Idara ya teknolojia bidhaa za ngozi Leonard Mayunga amesema chuo hicho kimekuwa kikizalisha vijana wenye ujuzi ambao waajiriwa na kujiajiri wenyewe.
Mayunga amefafanua kuwa kiwanda cha Kilimanjaro Moshi nguvu kazi kubwa imetoka katika Chuo DIT campu ya Mwanza na kwamba vijana wao wanapomaliza wanapata ajira katika taasisi na viwanda vilivyopp hapa nchini.
Amesema kuwa katika maonesho hayo wamekuja na bidhaa mbali mbali za ngozi zikiwamo viatu,mipira, wallet, mikanda ambaye inazalishwa katika Chuo cha DIT campus ya Mwanza.
Mayunga akizungumzia upatikanaji wa malighafi amesema Tanzania katika Bara la Afrika inashika nafasi ya pili kwa kuwa na mifugo mingi hivyo malighafi hapa nchini inapatikana.
Kwa upande wa bidhaa za mipira amesema wamekuwa wakifanya kazi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),ambapo hivi karibuni shirikisho hilo lilipaleka watu kutoka mikoa mbalimbali ili kujifunza kutengeneza mipira.
"Soko la mipira lipo tayari tumeshanza kuuza katika timu za mpira zilizopo Jijini Mwanza naamini hata timu kubwa kama Simba na Yanga nao watakuja tuwauzie bidhaa hii imetengenezwa kwa ustadi mkubwa," amesema Mayunga.
Akizungumzia changamoto walizonazo amesema kuwa sasa wanatumia mashine za kizamani huku akisema kuwa siku za usoni wanatarajia kuwa na mashine za kisasa.
0 Comments