Na Asha Mwakyonde,Dodoma
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania (KTO), linafanya kazi kama mwamvuli katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC), pia Shirika hilo linaundwa na wananchama ambao wanatoka katika FDCs ambapo lina program tatu ambazo ni 'Elimu Haina Mwisho (EHM)', Malezi na Makuzi pamoja na program ya Mpira fursa.
Akizungumza jijini Dodoma Aprili 26 kwenye maonesho ya wiki ya Ubunifu Kitaifa (IWTZ), ambayo yanaendelea kufanyika katika viwanja vya Jamuhuri yenye kaulimbiu isemayo 'Ubunifu Kwa Uchumi Shindani' Afisa Mawasiliano kutoka Shirika hilo Symphrose Makungu amesema program hizo wanaziendesha katika Vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, ambapo wanavisaidia katika maeneo mbalimbali yakiwa mafunzo na vifaa lengo likiwa ni kuhakikisha vinafanya kazi vizuri.
Makungu ameongeza kuwa Vyuo hivyo hapa nchini vipo 55 kati ya hivyo 54 vipo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kimoja kipo chini ya TAMISIMI.
Ameeleza kuwa Vyuo hivyo vinasaidiwa na serikali ambapo vimekarabatiwa na vinafundisha vizuri na kwamba programu wanazoziendesha zimesaidia kuongeza idadi ya washiriki hasa wanawake.
" Tupo hapa kwenye maonesho na Vyuo vya wananchi Ili kuhakikisha tunafikisha vizuri zile program tunazozisimamia tunazifikisha kwa jamii ili iweze kuzijua," ameeleza Afisa huyo.
Akizungumzia programu ya Elimu Haina Mwisho mbayo ni program mama na ni maalumu kwa ajili ya kuendeleza maarifa kwa wanawake vijana waliokatiza masomo kwa sababu mbalimbali zikiwamo ujauzito, kuugua, kukimbia kukeketwa lengo ni kuhakikisha Wanawake vijana wanatimiza ndoto zao kielimu.
Amefafanua kuwa kijana huyo anapojiunga na FDC anapata fursa ya kusoma masoma ya sekondari kwa mfumo usio rasmi ambapo atasoma masoma ya sekondari kwa miaka miwili kidato cha kwanza na cha pili kwa mwaka mmoja na Cha tatu na Cha nne mwaka mmoja.
Makungu ameeleza kuwa washiriki WA programu ya EHM ambao wanafanya vizuri wanapata nafasi ya kuendelea na kidato cha tano na sita katika shule za sekondari za serikali.
Akizungumzia gharama Afisa huyo amesema kuwa hakuna gharama yoyote atakayotozwamshiriki anachotakiwa ni kuwa na nia ya kusoma na kujilipia mahitaji yake binafisi yakiwamo nauli, mavazi na madaftari ada ya mafunzo ni bure.
"Mwanafunzi huyu atasoma masoma ya sekondari, ya ufundi, ujasiriamali na stadi za maisha. Lengo kuu la program ni kuhakikisha huyu binti anafikia malengo yake. Programu hii ilianza tangu 2018 tulianza na Vyuo vitatu hadi kufikia mwaka jana vikawa Vyuo 54,"amesema.
Amesema tungu program hiyo imeanza zaidi ya mabinti 9500 wamenufaika na program hiyo ya Elimu Haina Mwisho na kwamba mwaka huu waliojiunga ni zaidi ya wasichana 1267.
Makungu amesema kuwa programu huyo ni ya serikali hivyo hata ikitokea shirika la KTO halipo Vyuo hivyo vitaendela na programu.
0 Comments