VETA DODOMA YABUNI MFUMO WA UZALISHAJI UMEME UNAOONYESHA NISHATI


Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

WABUNIFU wawili ambao ni wanafunzi  wa Chuo cha VETA Dodoma, wametengeneza mfumo wa uzalishaji umeme unaoonyesha uzalishaji wa nishati hiyo  unaosafirishwa kutoka kwenye chanzo cha maji hadi kupata nishati ya umeme hadi kumfikia mtumiaji.

Akizungumza na mtandao huu kwenye maonyesho ya Wiki ya Ubunifu yaliyoanza April 24 na kutarajiwa kuhitimishwa April 28 mwaka huu,mwanafunzi Godwin Justine amesema,mfumo wameutengeneza  mfumo kwa kushirikiana na mwenzake Patrick ambao wote wanasoma fani ya umeme (Electronics).


Godwin amesema,lengo  kutengeneza mfumo huo ni  kutokana na maswali mengi kutoka kwa wanafunzi ambao licha ya kujifunza fani hiyo walitaka kujua namna umeme unavyopatikana hadi kumfikia mtumiaji.

Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo,mfumo huo sasa utakuwa mkombozi kwani utatumika kufundishia wanafunzi wa fani ya umeme na kuwawezesha kuelewa kwa urahisi kwani watakuwa wanaona na uhalisia wa kile wanachojifunza.

“Kumekuwa na changamoto ya uelewa katika kujifunza hasa unapojifunza wakati huoni uhalisia wake,sisi tukaamua kuunda mfumo huu ambao sasa unakwenda kuwarahisishiawanafunzi kujifunza , kuujua na kuuelewa umeme kwa undani na kuwajengea umahiri zaidi wa fani hiyo.”amesema Godwin.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA