RC SENYAMULE AFURAHISHWA NA MAONESHO YA MWAKA HUU


 Na Asha Mwakyonde, Dodoma

MKUU wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewashauri wananchi wa Mkoa wa Dodoma na wanaotoka mikoa ya jirani kutembelea maonyesho ya wiki ya Ubunifu Kitaifa (IWTZ),lengo likiwa ni kujifunza kupitia maonesho hayo na kuona kazi zinazofanywa na watanzania yanayoendelea katika viwanja vya Jamuhuri jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mabanda katika maonyesho hayo ziara iliyoenda sambamba na Siku ya VETA ,Senyamule amesema,ameshuhudia ubunifu unaofanywa na watanzania huku akisema ni kazi nzuri .

“Nimeshuhudia mambo makubwa ambayo wakifika hapa kutemebelea mabanda watayafahamu kupitia maonyesho haya.”amesema Senyamule

Aidha ameipongeza Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kuandaa maonyesho hayo ambayo mwaka huu yana sura ya Kimataifa kwani yameshirikisha wabunifu kutoka nje ya nchi.


“Nimeona wenzetu kutoka Afrika Kusini wametengeneza App inayomwezesha mama mjamzito kuangalia na kujifunza na kupata mahitaji yote yanayohitajika pindi mama anapokuwa mjazito ,tunaona hili jambo jema ambalo litasaidia kuunga mkono jitihada za Serikali za kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga ,kwa hiyo tunaomba teknlojia hii ibaki Tanzania.”amesisitiza Senyamule.

“Nimenunua bidhaa hii ni kutokana na kushuhudia ubora wake ,na nilitamani kununua vitu vingi zaidi,kwa hiyo nawasishi watanzania mjitokeze kwa wingi kushuhudia kazi zinazofanywa na watanzania.”ameeleza.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA