VETA SONGEA YABUNI MASHINE YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI


Na Asha Mwakyonde, Dodoma

MHITIMU wa kuchomelea kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA ), Chuo cha Mafunzo stadi VETA Songea, Savio Mapunda amebuni mashine ambayo inatumika kutengeneza chakula cha samaki.

Akizungumza Jijini Dodoma Aprili 25 katika banda la mamlaka hiyo kwenye maonesho ya wiki ya Ubunifu Kitaifa  (IWTZ), yenye kaulimbiu isemayo 'Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kuchangia Uchumi wa Bluu' ambayo yanaendela katika viwanja vya Jamuhuri Mapunda amesema baada ya kuchanganya mchanganyiko mashine hiyo hutumika kukata punje ndogo ndogo kulingana na umri wa samaki.

Ameongeza kuwa mashine hiyo inasaidia kutengeneza chakula hicho kuwa katika muonekana wa tambia na kukata kata.

Mapunda ameeleza kuwa  lengo la kubuni mashine hiyo ni  kuwarahisishia wafugaji wa samaki na kuisaidia jamii kupunguza gharama ya kwenda kununua vyakula vya samaki na badala yake wanunue kwa gharama nafuu.


Akizungumzia upatikanaji ma malighafi za kutengeneza mashine hiyo Mapunda amesema baadhi ya malighafi zilitotumika wamenunua na nyingine wamepata chuoni hapo

"Kutengeneza mashine hii imechukua muda wa wiki mbili kukamilika  na imegharimu kiasi cha fedha shilingi laki mbili na nikiipeleka sokoni nitaiuza kwa shilingi laki mbili na nusu," amesema.

Amewataka vijana wenzake kuacha tabia ya kukaa nyumbani na badala yake wakasome VETA ili kupata elimu ambayo itawasaidia kujiajiri wenyewe na kuinua uchumi wa nchi.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU