WATU BILIONI 1.2 WAMEJIHUSISHA NA FILAMU YA ROYAL TOUR


Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

 FILAMU  ya Tanzania ya 'The Royal Tour' imeingia kwenye mitandao mitatu mikubwa ya kidunia na ni ya tisa (9), kuandaliwa duniani na katika nchi za Afrika  ni ya pili ambapo imeoneshwa kwa kiwango cha asilimia 81.

Pia filamu hiyo imeleta mafanikio makubwa kupitia utalii ambapo kuanzia Januari 2022 hadi Disemba  waliongezeka watalii 600,020 sawa na asilimia 57.1

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Aprili 28,2023,wakati wa kuyatangaza mambo 10 katika mafanikio ya filamu ya Royal Tour kwa kipindi cha mwaka mmoja, Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kuitangaza Tanzania Kimataifa, Dk.Hassan Abbas ameeleza kuwa hadi kutangaza mafanikio hayo wastani wa takribani watu bilioni 1.2 wamejihusisha filamu hiyo.

Mwenyekiti huyo amefafanua kuwa watu bilioni 1.2 waliojihusisha na filamu hiyo ni pamoja na kuijua, kuiskia, kuiona au kuifuatilia Tanzania kutokana na Royal Tour.


Dk.Abbas amesema watu milioni 100 wameitazama filamu ya Royal Tour na kwamba uwekezaji wa ndani umeongezeka ambapo ilisainiwa mkataba yenye thamani ya Trillioni 8.

" Kumeibuka hamasa ni kama vile tumeenda kuniambia dunia kuwa tupo hapa, kwa mujibu wa Ripoti ya Waandaaji wa Royal Tour filamu hii imeshaoneshwa katika vituo zaidi ya 350 vya Runinga vilivyoko kwenye majimbo (States) zote za Marekani.

watalii waliotembelea maeneo mbalimbali nchini wameongeza mapato yatokanayo na sekta hi kutoka Shilingi trilioni 3.301 mwaka 2021 hadi Shilingi trilioni 5.8 mwaka 2023," amesema.

Ameongeza kuwa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni kufikia watalii milioni 5 hadi mwakani na  kwa mujibu wa ilani  hiyo wanatakiwa kufikia bilioni 6 ambapo  kwa sasa wapo nusu ya lengo huku akisema kuwa idadi ya ndege za Kitaifa zimeongezeka.

Filamu ya Royal Tour ilizinduliwa mjiini Arusha Aprili 28. mwaka jana.


Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU