MFUMO WA UTUMISHI NA e-GA UTAKAVYORAHISISHA UTENDAJI KAZI WA UMMA

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

OFISI ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao ( e-GA) imejipanga kutumia mifumo ya teknolojia kurahishisha utendaji kazi wa watumishi wa umma.

Akizungumza Jijini Dodoma Aprili 28,2023 na waandishi wa habari kwenye banda la e-GA wakati wa kilele cha Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yenye kaulimbiu isemayo 'Ubunifu Kwa Uchumi Shindani' Afisa TEHAMA kutoka Utumishi Hossea Laizek, ameeleza kuwa kuna mfumo wa watumishi portal ambao unaweza kuwahudumia watumishi wa Umma bila ya kufika katika kituo cha kazi ikiwa ni pamoja na kufanya uhamisho

Laizek amesema  kupitia mfumo wa E mrejesho watumishi  wanaweza kufuatilia taarifa mbalimbali kuhusu malalamiko, pongezi na huduma mbalimbali zinazotolewa katika ofisi.

Ameongeza kuwa kuna huduma nyingine inawezesha watumishi kupanga mipango  yao ya  mwaka na kurekodi utendaji kazi wake wa  kazi.

Afisa TEHAMA  kutoka  Mamkala Mtandao (e-GA)  Tumaini Masinsi amesema kupitia maonesho hayo kuna  mfumo uitwao Oxgen Net ambao ni wa Whatsup ya ndani.

“Oxgen ni chatting platform ni ya hapa ndani kwa ajili ya kuchat na kwa ajili ya video Call na kwa ajili ya kujifunza vitu mbalimbali na kwamba upatikanaji ni wa kutumia Web Oxgen Net na kuitumia na katika  Playstore.

"Katika maonesho haya tumeja na bunifu mbalimbali za mfumo kwenye mambo ya tehama ambazo zimefanywa na vijana wabunifu.


Naye,Afisa TEHAMA kutoka Mamlaka Mtandao Vannesa Mhando  amesema wao kama vijana wanajifunza uzalendo na kutiwa moyo kuendelea kutengeneza suluhu ambazo zitatua matatizo ya watanzania.

Amesema wanajiendeleza kiteknolojia kwa ajili ya kukuza ujuzi na kuendeleza mambo mazuri na kwamba wameonesha suluhu mbalimbali za mifumo ambayo itapunguza gharama kubwa na kubwa ambayo imefanywa na wazawa.









Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA