TAEC YATAKIWA KUWEKEZA KATIKA UTAFITI WA NYUKLIA


Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

TUME ya nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC),imetakiwa kuwekeza zaidi katika utafiti ili kupata bunifu nyingi hasa kwenye eneo la Sayansi ya Nyuklia kwani ni muhimu  katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.

Mkurugenzi wa idara ya sayansi na teknolojia kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Maulilio Kipanyula ametoa wito huo leo Jijini Dodoma kwaniaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya elimu wakati wa siku ya atomiki kwenye maonyesho ya wiki ya ubunifu iliyoambatana na maandamano yaliyofanyika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi wa Tume hiyo,Prof Joseph Msambichaka ameitaka tume ya Atomiki kufanya bunifu nyingi zinazotokana na nyuklia kwani Tume hiyo ina uhitaji wa vifaa vingi vyakutosha.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Atomiki Prof Lazaro Busagala amesema kuwa hapo baadae wanatarajia kuwa na uwakilishi mkubwa wa wanawake katika sayansi na teknolojia hasa ya nyuklia ambapo hivi sasa wametenga jumla ya Shilingi bilioni 2.6 kwaajili ya kuwasomesha wanafunzi ambao wamefanya vizuri katika shahada zao kupitia mpango mkakati wa dokta Samia scholarship ili kupata wabunifu zaidi.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA