SPIKA WA BUNGE DK.TULIA AIPONGEZA TTCL KWA KUPANUA HUDUMA ZAKE


 Na Asha Mwakyonde,Dodoma

SPIKA wa  Bunge la Tanzania Dk.Tulia Ackson amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL),
kwa hatua iliyofikia ya kuwapelekea wananchi huduma za mtandao nyumbani  na sio tu kwa taasisi mbalimbali kama ulivyokuwa awali.

Hayo ameyasema Jijini Dodoma leo Mei 18,2023 katika viwanja vya Bunge kwenye maonesho ya watoa huduma za mawasiliano yalioandaliwa na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Tulia amesema mkongo wa Taifa wa mawasiliano unakwenda kumfikia mwananchi mlangoni kwake ni jambo la misingi na muhimu katika kurahisisha uchumi wa kidigitali.

" Nichukue fursa hii kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya nimepita hapa kwenye mabanda machache nimeona kazi ni nzuri pia niipongeza sana Wizara yetu ya habari kwa kuweza kuleta maonesho haya  hapa bungeni ili wabunge tuweze kujionea wenyewe mambo yanayoendelea katika maeneo yetu ya uwakiliahi," ameongeza.

Pia nimeoneshwa mambo mengi likiwamo la mkongo wa Taifa wa mawasiliano ambao unaenda kumfikia mwananchi mlangoni kwake," ameeleza Spika Dk.Tulia.

Dk. Tulia ametumia fursa hiyo kulipongeza Shirika hilo kwa hatua waliyofikia kupeleka huduma majumbani  na sio tu kwa taasisi mbalimbali  huku akisema kuwa anaamini  huduma hizo zitapunguza gharama za matumizi ya bando ambayo huwa wananchi wanalalamika hapa na pale.

"Nasikia na nimeona kwenye vyombo vya habari mmefika mlima Kilimanjaro nami ningefurahi siku napanda kule ,muwe meshaweka na madamu mmeweka nitajipanga vizuri niende kupanda mlima Kilimanjaro nitakuwa na uhakika wa mawasiliano hadi ninaoofika kileleni" amesema Dk.Tulia.


Ameeleza kuwa kutokana na mawasiliano kufikia katika mlima Kilimanjaro hakutakuwa na  uongo uongo lazima mtu apige video ili kujua amefika au hajafika tofauti na awali hadi akishuka ndio anaanza kuposti picha za kileleni.

Aidha amewapongeza TTCL kwa hatua  hiyo ya mawasiliano kuweza kufika kilele cha juu zaidi duniani kwa mlima Kilimanjaro ambao umesimama peke yake.

Akizungumzia Shirika la posta amesema kuwa linatakiwa kuongeza nguvu zaidi kwa kuwa limewezeshwa na anwani za makazi.

Amesema kuwa amefurahishwa na zoezi la anuwani za makazi ambalo lilianzia mapema mwaka jana na kwa sasa wamefikia sehemu ambayo kwa yule aliyesajiliwa namba yake anaweza kuipata kiganjani kwa kutumia aina yoyote ya simu.

"Nitumie fursa hii kuwapongeza kwa juhudi mbalimbali ambazo zinafanywa na Wizara hii ya habari mtu kujua anwani yake ya makazi ni jambo la msingi sana.,"ameeleza.

Aidha amewataka wananchi ambao bado hawajasajili makazi yao ni muhimu kupata anwani za makazi  ambazo zinasaidia katika maendeleo.


Kwa upande wake Meneja Biashara TTCL, Mkoa wa Dodoma ,Leyla Pongwe amesema kuwa Shirika hilo katika kuchagiza agenda ya serikali ya kiuchumi wa kidigitali  ifikapo 2025 wameenda bungeni kuonesha mikakati waliyonayo.

"Tumekuja katika viwanja vya Bunge kuwaonesha wabunge mkakati tulionao  katika kuisaidia serikali kufikia uchumi wa kidigitali ifikapo 2025," ameeleza.

Ameongeza kuwa TTCL wameweza kurahisisha utalii baada ya kufikisha mawasiliano kilele cha Uhuru Park katika mlima Kilimanjaro ikiwa ni miaka 61 ya uhuru.

Meneja huyo amefafanua kuwa Uhuru Park ni kilele  cha Afrika Mashariki huku akisema awali mtalii alikuwa akipanda kwenye mlima huo simu yake  haikuweza kupatikana hadi atakaposhuka kutoka mlimani.

Amesema kwa sasa mtalii huyo anaweza kupatikana kila kituo atakapokuwa amefika na kwamba wanahuduma ya faiba mlangoni kwako bure mteja anatakiwa kulipia kifurushi cha mwezi.

"Tunajua kuwa ili ufikie uchumi wa kidigitali lazima uwe na mtandao imara na hapa tumeweza kuwaonesha wabunge kwamba ukiwa na mtandao wa faiba wa TTCL una uwezo wa kuwasiliana na kufanya vitu hata ukiwa mbali unaweza kuiona nyumba yako kupitia 'application' ya simu," amesema Meneja huyo.

Amesema kuwa wameweza kufikisha mkongo wa Taifa hata katika mipaka yote ya Tanzania na kwa sasa wameanza kutoka nje ya Tanzania ili kufikisha mawasiliano ya faiba kwenda katika nchi za jirani za Afrika Mashariki.

Post a Comment

0 Comments

 MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI