GCLA:FAHAMU SABABU ZA MTOTO KUZALIWA NA JINSI ZAIDI YA MOJA

Na Asha Mwakyonde Dar es salaam

MTOTO kuzaliwa na jinsi zaidi ya moja  Kibaiolojia, kimaumbile baada ya mimba kutunga kuna mwendelezo wa kiumbe kukua na ukuaji wa kiume hicho hutengemea vitu mbalimbali viweze kumsaidia mtoto huyo kukua vile ambavyo inatakiwa.

Akizungumza Jijini Dar es salaam Julai 8,2023 Meneja Maabara ya Sayansi Jinai,Baiolojia na Vinasaba kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA),Fidelis Bugoye katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji,"  amesema, maumbile ya mtoto kukua kuna homoni na mwingiliana wa vinasaba ambavyo mtoto huyo amerithi kutoka kwa wazazi wake.

Amefafanua kuwa homoni hizo zikiwa na changamoto mbalimbali, katika mpangilio wa vinasaba inaweza kusababisha mtoto jinsi zaidi ya moja.

Bugoye ameeleza kuwa uchunguzi wa vinasaba unaweza kufanyika kubaini jinsi tawala (Dominant sex), kwa sababu anaonekana wakike au wakiume ukifanya uchunguzi wa vinasaba.

"Sisi tuna utaalamu na mitambo ambayo ikifanya uchambuzi wa vinasaba (DNA analysis), tunaweza kubaini ni wakike kama mpangilio wa DNA unakuwa XX, Lakini mpangilio wa vinasaba eneo hilo ukiwa XY basi itakuwa mtoto huyu ni wa kiume," Bugoye.

Meneja huyo akizungumzia maonesho hayo amesema kuwa watu wengi wanaotembelea banda Maabara hiyo wanataka kujua huduma zinazotolewa na mamalaka hiyo hususan kwenye eneo la kupima vinasaba (DNA).

Ameeleza kuwa wao kama mamlaka hiyo wanawaeleza  kuwa kwa mujibu wa sheria kifungu namba 25 anayehitaji kupata huduma ya kupima DNA muhusika atanzania aidha Ustawi wa jamii, kwa mawakili, mahakama kama jambo hilo linamgogoro na kama linahusiana na tiba atawakilishwa na madaktari.

Bugoye amesema Maabara hiyo inafanya kazi mbalimbali za uchunguzi wa sampuli za Sayansi jina, kibaiolojia na vinasaba kwa lengo kufanya utambuzi wa binadamu.

"Katika maonesho haya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu imeleta Wataalamu kwa lengo la kutoa elimu kwa wadau na wananchi mbalimbali ili kuzifahamu shughuli zinazotekelezwa na Maabara hii ," amesema Bugoye.

Ameongeza kuwa pamoja na kauli mbiu ya mwaka huu Mkemia Mkuu wa serikali amewa weletea wananchi ujumbe, wadau wake ambao ni 'Matumizi sahihi ya Kemikali na Matumizi ya Sayansi ni Nguzo muhimu katika Biashara na Uwekezaji'.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU