Na Asha Mwakyonde,Dar es salaam
MATUMIZI ya Teknolojia kwa wafanyabiashara ni muhimu katika kurahisisha shughuli zao za kibiashara hasa kwa upande wa mawasiliano katika uzalishaji mali hivyo hayakwepeki.
Akizungumza jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila alipotembelea Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Sabasaba July 11, 2023 katika viwanja vya Mwalimu JK Nyerere Temeke Jijini Dar es Salaam, amesema ulimwengu wa sasa ni wa sayansi na teknolojia hivyo wafanyabiashara wanapaswa kujikita zaidi kwenye teknolojia hiyo ili kuwarahisishia shughuli zao za kibiashara.
Chalamila ameongeza kuwa katika maonesho hayo wameona ni kwa namna gani teknolojia hiyo ilivyobeba shughuli mbalimbali katika sekta za kilimo, habari.
Amesema kuwa lazima taasisi za uzalishaji na utoaji huduma nchini zibadilike ili kutumia vyema mabadiliko hayo ya sanyansi na teknolojia katika shughuli zao.
"Tumeona wenzetu Wachindi namna ambavyo teknolojia hii imetumika kwa kiasi kikubwa na imekuwa ni pendezesho kwenye maonesho haya na kwa sasa baada ya teknolojia hiyo kuwa imekwishaonwa kilichosalia ni kuihamisha ili iweze kufanya kazi katika nchi yetu ya Tanzania.” amesema Chalamila.
Amewashukuru viongozi Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi kwa kuwakaribisha wawekezaji mbalimbali wa ndani wa kigeni pamoja na kurahisisha shughuli za uwekezaji na ufanyaji biashaa nchini.
0 Comments