TANESCO YAONGEZA MAUZO YAFIKIA TRILIONI 1.8

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO),limeongeza mauzo ya umeme katika kipindi cha miaka miwili kutoka Sh trilioni 1.6 mwaka 2020/2021 na kufikia Sh trilioni 1.8 mwaka 2021/2022 sawa na asilimia 11.

Hayo yamesemwa leo Julai 27,2023 na Mkurugenzi wa Fedha Tanesco, Renata Ndege, wakati wa kikao kazi cha uongozi wa shirika hilo, Msajili wa Hazina na Wahariri wa vyombo vya Habari kuelezea mafanikio ya mwaka 2021/22, ameeleza kuwa mwaka jana wamepata faida Sh bilioni 109.4 kutoka Sh bilioni 77 za mwaka 2021 ongezeko aslimia 42.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa
wameongeza uzalishaji ikiwa ni pamoja na  kuongeza wateja na kwamba kwa sasa Shirika hilo halitengenezi  hasara bali limekuwa likitengeneza faida.

"Hii inatokana na maboresho ya fedha mwaka hadi mwaka yanayoendelea kwa sasa shirika hili halitengenezi  hasara bali  limekuwa faida," ameeleza.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Maharage Chande, amesema utekelezaji wa mradi wa uzalishaji umeme katika Bwawa la Julius Nyerere umefikia asilimia 90 na kwamba Juni 2024 watawasha umeme.

“Mradi huu ni muhimu kwa sababu unagharimu Dola zaidi ya bilioni 3.5 na umeme huu ukipatikana utatosheleza mahitaji hata zikiungwa nyumba zote Tanzania,” amesema Chande.

Aidha amesema kulikuwa na malalamiko mengi ya wafanyakazi na kuthibitishwa kutokuwa na mikataba lakini hivi sasa wametatua na kuboresha muundo wa utumishi.

Kwa mujibu wa Chande, kila mwaka wanachagua wafanyakazi 20 kutokana na utendaji wao kisha kuwapeleka kwenye mafunzo nje ya nchi ambapo huwaunganisha kwenye kampuni kubwa ili kuwaandaa kurithi nafasi mbalimbali ndani ya shirika hilo.


Amesema hivi sasa watu 20 wako Afrika Kusini na tayari wameingia makubaliano na nchi nyingine kama Algeria kupeleka wafanyakazi kupata ujuzi zaidi.

“Tumeandaa ‘Graduate trainee programme’ ambapo kila mwaka tutauwa tukichukua wanafunzi 50 wa vyuo vikuu kwa ajili ya kuwapa mafunzo zaidi. Kutokana na hizi program miaka mitatu baadaye tunaamini watu watakuwa na hamu ya kuja kufanya kazi Tanesco,” amesema Chande.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amelipongeza shirika hilo kwa kazi kubwa inayofanya na kusema ni taasisi ya mfano wa kuigwa.

Shirika hilo lenye wateja milioni 4 limewaunganishia umeme wateja wapya 504,366 kwa mwaka 2021/22.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI