AMKENI SACCOS YAJIVUNIA MAFANIKIO, YAWAKARIBISHA WANACHAMA


Na Asha Mwakyonde, Mbeya

WANANCHI WA Jiji la Mbeya wameshuriwa kujiunga na 
Chama cha Akiba na Mikopo Amkeni LTD, (SACCOS), ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kupata mikopo yenye riba nafuu.

Akizingumza jijini Mbeya leo Agosti 4, 2023, katika banda lao lililopo ndani ya kijiji cha ushirika 
Mwenyekiti wa SACCOS hiyo Remigia Mbaga kwenye maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane nane), ambayo yanafanyika Kitaifa mkoani hapa katika viwanja vya John Mwakangale yenye kaulimbiu isemayo 'Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula', amesema Chama hicho kinatoa mikopo Kwa wanachama wake lengo likiwa ni kuwakomboa kiuchumi.

Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa chama hicho Januari mwaka 2009 kina wanachama 233 ambapo kilianza na wanachama 34.

Ameongeza kuwa  wanachama wake baada ya kujiunda na SACCOS hiyo wamebadilisha maisha yao ambapo wamepata mafanikio mbalimbali yakiwamo kujenga nyumba, kusomesha watoto wao pamoja na kuanzisha biashara zenye tija.

"Tumekuja hapa kuonesha kazi tunazozifanya na kuwahamasisha wananchi kujiunga na chama hiki ambacho ni mkombozi kiuchumi," amesema mwenyekiti huyo.


Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA