Na Asha Mwakyonde,Mbeya
VYAMA vya ushirika vya akiba na mikopo vimetakiwa kutumia huduma inayotolewa na Kampuni ya VERIDOC Global Tanzania zikiwamo za kusaini mikataka ya kidigitali na kuweka alama za utambuzi kwenye nyaraka muhimu.
Akizingumza jijini Mbeya leo Agosti 4, 2023, Afisa Masoko kutoka Kampuni ya VERIDOC Global Tanzania Swamiath Tizetwa
kwenye maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane nane), ambayo yanafanyika Kitaifa mkoani hapa katika viwanja vya John Mwakangale yenye kaulimbiu isemayo 'Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula', wakati akitoa maelezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa,Gerald Kusaya alipotembelea banda chama hicho lililopo ndani ya Kijiji cha ushirika.
Amesema kuwa shughuli kubwa wanazozifanya katika vyama vya ushirika ni kusaini mikataka ya kidigitali na kuweka alama za utambuzi kwenye nyaraka zao.
Tizetwa amefafanua kuwa kazi nyingine ni kutoa suluhisho la vifungashio na kuweka alama za utambuzi kwenye bidhaa zao
" Pia tuna uza vifaa vya TEHAMA kwenye vyama vya ushirika zikiwamo simu za mkononi, printa, kompyuta mpakato na mizani pamoja na kutoa elimu ya kitehama kwa vyama hivyo," amesema.
Mtoa huduma huyo ameeleza kuwa wanatoa mifumo ya kimahesabu kwa vyama vya kuweka akiba na mikopo saccos na vyama vya msingi AMCOS.
0 Comments