BRELA YATAKIWA KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA


Na Asha Mwakyonde, Mbeya

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe,ameeleza kuwa  licha ya kuwapo kwa changamoto ya mtandao katika kufanya usajili ‘online registration system’ lakini kuna maboresho makubwa yaliyofanywa na Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Pia ameitaka  BRELA kuendelea kushirikiana na taasisi nyingine lengo likiwa nu  kurahisisha utoaji huduma zake kuwapo kwa mabadiliko ya mifumo mbalimbali ukiwemo mfumo mpya wa Tausi.

Naibu Waziri huyo ameyasema hayo  jijini Mbeya leo 5, 2023, alipotembelea banda la BRELA katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane nane), ambayo yanafanyika Kitaifa mkoani hapa katika viwanja vya John Mwakangale yenye kaulimbiu isemayo 'Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula', ameeleza kuwa malalamiko makubwa yako kwenye leseni daraja B ambazo zinatolewa na halmashauri.

Aidha ameutaka Wakala huo kuendelee kuboresha mifumo ili wananchi wasipate vikwazo katika kufanya biashara zao.


"Tuangalie  namna ya kuiboresha mifumo yetu ili isomane na taasisi nyingine mtu anapotaka kuingia kwenye mfumo aone na taasisi nyingine anayotaka," amesema Kigahe.

Kwa upande wake Mkuu wa Uhusiano BRELA, Roida Andusamile, amesema Wakala huo una mpango wa kuhuisha mifumo yake na mingine ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.

"kuna mpango ambao utatuwezesha ili mifumo hii iweze kusomana na ikisomana urasimu utaondoka kwa watu tunaowahudumia,” amesema.

Post a Comment

0 Comments

ENDELEENI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA VIRUSI VYA UKIMWI” MHE. NDERIANANGA