MAMCU LTD IMELIPA SH.BILIONI 147.7 VYAMA VYA MSINGI, YAONGEZA MBAAZI

Na Asha Mwakyonde, Mbeya

CHAMA Kikuu cha Ushirika Masasi Mtwara (MAMCU LTD), kimewaondolea wakulima wa korosho changamoto ya kutaka  kuuza mazao kabla ya kuyapeleta kwenye chama hicho ambapo kimelipa zaidi ya Sh bilioni 147.7 katika msimu wa mwaka 2021/22 kupitia vyama vyao vya msingi.

MAMCU LTD  imenunua mbegu za ufuta tani 10 zenye thamani ya Sh milioni 65 na kuzigawa kwa wakulima lengo likiwa ni kuhakikisha wanapata bei nzuri kwa kuzalisha ufuta mweupe.

Akizungumza Agosti 6, 2023 katika Kijiji cha Ushirika kilichopo kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya,yenye kaulimbiu isemayo 'Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula',Ofisa Kilimo wa chama hicho, Martha Shirima, amesema
kuna changamoto za wakulima kutaka fedha kwa haraka.

Ofisa huyo ameeleza kuwa Chama hicho kinaendelea kufanya maboresho ili mkulima asiwe na haraka ya kuuza mazao yake kwa mtu mwingine na badala yake apekeke kwenye chama.

"Katika  mwaka 2022/23 chama kimeuza  kilo 59,607,667 kwa thamani ya Sh 111,449,764,229 kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ambapo bei ya juu ilikuwa Sh 2,200 na ya chini Sh 1,700," ameeleza Shirima.


Akizungumzia  mafanikio ya MAMCU LTD,  amesema   imefanikiwa kudhibiti ubora wa korosho kwa kununua vipima unyevu 175 na mizani ambapo ziligawiwa  kwa wakulima ili kuwawezesha kujua unyevu wa korosho kabla ya kupelekwa kuhifadhiwa kwenye maghala makubwa.

"Chama hiki hakihudumii mazao ya korosho tu bali kinahudumia mazao ya ufuta pamoja na mbaazi, msimu wa mwaka 2023 kimeuza kilo 17,111,270 za ufuta kwa thamani ya Sh 61,261,338,927 na bei ya juu ilikuwa Sh 3,967 kwa kilo na ya chini Sh 3,560," amesema.

Ofisa huyo amesema wanatarajia mwezi  huu Agosti 11  kuwa  mnada wa kwanza wa zao la korosho kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa kuwa chama kimekua.

Mbali na mafanikio hayo pia Chama h kimefanikiwa kujenga maghala makuu matatu katika Wilaya za Mtwara, Masasi na Nanyumbu lengo ni  kusogeza huduma karibu za kuhifadhi mazao kabla ya  mnada.

Post a Comment

0 Comments

DKT. BITEKO ASISITIZA UMUHIMU WA MIFUMO THABITI YA NISHATI JADIDIFU KUKIDHI MAHITAJI YA NISHATI