TIRDO YAKARIBISHA WAWEKEZAJI MAFUTA TETE


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe (kushoto), akiangalia mafuta Tete ya Parachichi alipotembelea banda la Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO),(kulia), ni Mtafiti kutoka TRIDO Paul Kimath  akitoa maelezo ya namba mafuta Tete  yanavyochakatwa.

Na Asha Mwakyonde, Mbeya

MTAFITI kutoka Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO),Paul Kimath, amesema Shirika hilo linatafuta wadau ili kuwekeza katika uzalishaji wa mafuta Tete ya parachichi hasa wajasiriamali wadogo,vikundi vya akina mama na vijana katika Halmashauri mbalimbali nchini.

Akizungumza jijini Mbeya leo 5, 2023, katika banda la TRIDO kwenye maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane nane), ambayo yanafanyika Kitaifa mkoani hapa katika viwanja vya John Mwakangale yenye kaulimbiu isemayo 'Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula', ameeleza kuwa lengo lao kwa sasa ni kuwatembelea na  kuwahamasisha  wadau hao ili  waweze kuanza kuzalisha mafuta hayo.

Mtafiti huyo amesema kuwa wamefanya tatifi nyingi mojawapo ni ya zao la Parachichi ambapo wamegundua kuongeza thamani katika zao hilo na kuona kwamba litakuwa na tija kwa wakulima wa kanda za Nyanda za Juu Kusini.

"Tupo hapa katika maonesho tumekuja na teknolojia tatu katika ukanda huu wa Nyanda za Juu Kusini tumekuja na teknolojia ya zao la Parachichi, tumetembea mikoa yote ya jirani ya Iringa, Njombe, Mbeya na Songwe tumeona soko la mazao ya parachichi linawapa shida," amesema.


Mtafiti huyo amesema wamebuni teknolojia ya mashine ya kuchakata mafuta ya parachichi kuanzia hatua ya mwanzo hadi ya mwisho ya upatikanaji wa mafuta hayo.

Amefafanua kuwa mafuta hayo yatokanayo na parachichi yanatumika katika matumizi mbalimbali yakiwamo kutumika kama mafuta ya kula, kutengenezea shampoo, mafuta ya kupaka kwa watu wa rika zote.

"Mafuta haya  yanavitamini A na vitamini E ambayo ni malighafi muhimu katika bidhaa za urembo,usafi kwa ujumla wake hivyo wananchi wa mikoa hii kilimo cha parachichi kuanzia mikoa ya Kilimanjaro, Iringa, Mbeya, Njombe na Songwe waje TRIDO kujifunza kuchakata mafuta haya na baadae wapate mashine hii," ameeleza.

Akizungumzia soko la mafuta ya parachichi amesema kwa ni kubwa ambapo lita moja inauzwa Sh. 25,000 kwa sasa na kwamba mafuta hayo yataendelea kupanda bei kulingana na mahitaji.

Ameongeza mashine ya kuchakata mafuta hayo inauzwa kwa gharama ya sh. Milioni 5.5 ambayo inajumuisha mashine na vifaa yake pamoja na mafunzo yanayolenga uchakataji wa mafuta hayo.

Post a Comment

0 Comments

DKT. BITEKO ASISITIZA UMUHIMU WA MIFUMO THABITI YA NISHATI JADIDIFU KUKIDHI MAHITAJI YA NISHATI