PROF. MKENDA APONGEZA JITIHADA ZA VETA

Na Asha Mwakyonde,Mbeya

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda
amekipongeza Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kwa namna ambavyo vijana wanavyojiari kupitia mafunzo ya vyuo vyake.

Pia ametoa maelekezo kwa taasisi mbalimbali nchini kuendeleza bunifu na kuziingiza sokoni ili ziweze kushindana katika soko la dunia.

Akizungumza  mara baada ya VETA kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, Profesa Mkenda ameeleza kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikitoa mafunzo yenye tija kwa vijana na kuweza kujiajiri pindi wanapomaliza mafunzo hayo.

Prof. Mkenda amesema maendeleo ya teknolojia yanayofanywa na taasisi za Serikali ni makubwa  na kwamba wanahitaji.

" Nimemuona mwanamke aliyepata mafunzo hapa VETA  ya kutengeneza simu na anafanya vizuri kule Kariakoo najiingizia kipato," ameeleza.

“Tunachohitaji vile vilivyogundulika visiwe tu vya maonesho mwaka huu au mwakani, tunataka tuvione vinaingia sokoni vinaanza kuuzwa," amesema Profesa Mkenda.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu Veta, Anthony Kasore, amesema wanawafundisha vijana ili kuwaandaa kuingia kwenye soko la ajira katika nyanja mbalimbali za uwekezaji, viwanda, kilimo na ufugaji.

“Tumekuja na bunifu kwa ajili ya kuwasaidia wakulima kufanya shughuli zao za kilimo na ufugaji kwa urahisi,” amesema Kasore.

Kwa mujibu wa Kasore, kupitia mradi wa sumu kuvu vijana 420 kutoka katika wilaya 20 wamepatiwa ujuzi wa kutengeneza vihenge ambapo Serikali itawapatia vifaa bure kuweza kujiajiri. 

Kaimu mkurugenzi huyo, amesema pia ujenzi wa vyuo vipya katika wilaya 64 na kimoja katika Mkoa wa Songwe utaongeza wigo wa mafunzo ya ufundi stadi kutolewa kote nchini.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU