Na Asha Mwakyonde, Mbeya
TUME ya Nguvu ya Atomiki Tanzania (TAEC), imetakiwa kuendelea kuelimisha umma kuhusu matumizi salama ya mionzi kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi hasa katika maeneo ya vijijini lengo likiwa ni kujilinda na madhara yatokanayo na mionzi hiyo.
Ushauri huo umetolewa Agosti leo 6, 2023 na Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Shamata Khamis, baada ya kutembelea banda la tume hiyo kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, ameeleza kuwa tume hiyo inatoa elimu hivyo hivyo ni vema ikawafikia wananchi waliopo vijijini.
"Ili kuwalinda na mionzi wananchi waliopo maeneo ya vijijini ni vema mkaenda kutoa elimu hii mnayoitoa hapa nao wape kujua madhara yake," ameeleza.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TAEC, Peter Ngamilo, ameeleza kuwa wanatumia mitandao ya kijamii kuhakikishia wananchi na kwamba elimu hiyo inawafikia ikiwa ni pamoja na kufanya vipindi vya kuelimisha kwenye vyombo vya habari mbalimbali kama redio na runinga.
"Mbali na elimu tunayoitoa hapa pia tunahakikisha wananchi wanafikiwa na elimu hii kwa kutumia mitandao ya kijamii," amesema.
"Mkuu huyo wa kitengo amebainisha kuwa endapo watabaini baadhi ya maeneo kuna mionzi iliyozidi wanawapeleka wataalam kuangalia na kama mionzi hiyo utakuwepo wanasimamisha huduma
Amesema kama kama wakikuta mashine mbovu wanasimamisha huduma hadi mashine hiyo itakapotengenezwa ndipo wataruhusu huduma iendelee.
Ameongeza kuwa baadhi ya majukumu ya Tume hiyo ni kunapima sampuli za mazingira kubaini uchafuzi wa mionzi kwenye mazingira, kupima kiwango cha mionzi kwenye minara ya simu na rada za mawasiliano, kukusanya, kusafirisha na kuhifadhi mabaki ya vyanzo vya mionzi.
0 Comments