Na Asha mwakyonde, Mbeya
WAKULIMA wameshauri kutumia Vihenge vinavyotengenezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),lengo likiwa ni kupata bidhaa bora inayotokana na Wakala huo.
Akizingumza jijini Mbeya leo 6, 2023, katika banda la Wakala huo
Meneja wa TBA ,Mkoa wa Mbeya Mhandisi Salum Chanzi kwenye maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane nane), ambayo yanafanyika Kitaifa mkoani hapa katika viwanja vya John Mwakangale yenye kaulimbiu isemayo 'Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula',amesema wameendelea kufanya kazi mbalimbali ikiwamo ujenzi wa vihenge kwa ajili ya wakulima ambavyo vimejengwa mkaoni Rukwa.
Mhandisi Chanzi amesema wamekuwa wakipata kazi za kukarabati maghala ya Shirikisho la vyama vya Ushirika (TFC).
Ameongeza kuwa TBA imeendelea kujiimarisha na sekta mbalimbali huku akitolea mfano viwanja cha Sokoine wanatarajia kukikarabati.
"Ushiriki wetu katika maonesho haya ni kuonesha nini tunatekeleza kwa wadau mbalimbali sekta ya majengo tumefika hapa ili sekta hizi ziweze kutambua kazi zetu na ziweze kushirikiana nazo katika sehemu mbalimbali.
Amesema kuwa wanatoa ushauri masuala ya ujenzi kwa taasisi za serikali.
Naye Mhandisi Ujenzi kutoka TBA, Mhandisi Haruna Kalunga amesema maghala hayo ni ya kisasa na ni mkombozi kwa mkulima.
Amesema kuwa TBA ilikuwa ni mshauri, muongoza mradi katika ujenzi wa vihenge na kwamba teknolojia iliyotumika imetoka nchini Poland ambapo walikuwa wakisaidiana na watu wa nchi hiyo.
Mhandisi Kulunga ameongeza kuwa wametekeleza teknolojia nzuri ambayo inaenda kumkomboa mkulima.
"Miaka ya nyuma mkulima alikuwa akivuna mahindi yake takribani asilimia 30 hadi 40 ilikuwa inapotea wakati wa uzalishaji," ameeleza.
Amefafanua kwa sasa mkulima akivuna mahindi yake katika vihenge hivyo kuna sehemu ya Maabara atapimwa kujua yanaunyevu nyevu kiasi na yana ubora gani.
Mhandisi huyo ameeleza kuwa kwenye vihenge hivyo kuna sehemu ya kuchagua badala ya
kupepeta mahindi, kukausha hadi kufikia kiwango kinachotakiwa.
Amesema Mradi huo ni mzuri unatunza mahindi pasipo kutumia sumu kama ilivyokuwa awali ambapo kwa kutumia Vihenge yanatunzwa kwa kutumia joto na likizidi inawashwa feni.
0 Comments