VERIDOC SULUHISHO KWA VYAMA VYA USHIRIKA YATOA HUDUMA KIDIGITALI


Na Asha Mwakyonde,Mbeya

VYAMA vya ushirika vya akiba na mikopo vimetakiwa kutumia huduma inayotolewa na Kampuni ya  VERIDOC Global Tanzania zikiwamo za kusaini mikataka ya kidigitali na kuweka alama za utambuzi kwenye nyaraka muhimu.

Akizingumza jijini Mbeya leo  Agosti 4, 2023, Afisa Masoko kutoka Kampuni ya VERIDOC Global Tanzania Swamiath Tizetwa,kwenye maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane nane), ambayo yanafanyika Kitaifa mkoani hapa katika viwanja vya John Mwakangale yenye kaulimbiu isemayo 'Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula', wakati akitoa maelezo kwa  Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa,Gerald Kusaya alipotembelea banda chama hicho lililopo ndani ya Kijiji cha ushirika.

Amesema kuwa shughuli kubwa wanazozifanya katika vyama vya ushirika ni kusaini mikataka ya kidigitali na kuweka alama za utambuzi kwenye nyaraka zao.

Tizetwa amefafanua kuwa kazi nyingine ni kutoa suluhisho la vifungashio na  kuweka alama za utambuzi kwenye bidhaa zao 

" Pia tuna uza vifaa vya TEHAMA kwenye vyama vya ushirika zikiwamo simu za mkononi, printa, kompyuta mpakato na mizani pamoja na kutoa elimu ya kitehama kwa vyama hivyo," amesema.

Mtoa huduma huyo ameeleza kuwa wanatoa mifumo ya kimahesabu kwa vyama vya kuweka akiba na mikopo saccos na vyama vya msingi AMCOS.


Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA