WADAU WAKUTANA KUJADILI MATUMIZI SAHIHI YA TAKWIMU

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

OFISI za Taifa za Takwimu barani Afrika zinawajibu mkubwa wa kusaidia nchi kufanya maamuzi yanayohusu sera kuhusiana na eneo huru la biashara afrika na kwamba takwimu hizo zinakuwa na maana pale ambapo zinatolewa taarifa kwa kuwa zinakwenda kukidhi mahitaji kwa usahihi na idadi husika.

Pia Ofisi ya Taifa Takwimu (NBS),na za Takwimu barani Afrika zinatakiwa kuendelea kuzalisha Takwimu rasmi na zenye ubora na kuzisambaza kwa njia rafiki na zakuaminika, kwa wakati lengo likiwa ni kuwezesha Serikali na wadau kufanya maamuzi yanayohusu utekelezaji wa eneo huru la biashara katika Bara hilo kwa wakati.

Hayo yamesemwa  jijini Dodoma jana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri wakati akifungua  kongamano la kitaifa  kuhusu maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika alilieleza kuwa wakati Ofisi hizo zikifanya hayo hazina budi kuboresha mifumo ya ushirikiano wa kitakwimu ili ziweze kuwafikia wadau kwa urahisi na kwa usahihi  kwa kuzingatia matumizi ya njia rahisi za usambazaji wa takwimu husika.


"Kongamano hili limebebwa na kauli mbiu isemayo "Uboreshaji wa mifumo ya ushirikiano wa kitakwimu ili kuharakisha utekelezaji wa eneo huru la biashara la Afrika(AFCFTA), mchango wa Takwimu rasmi na 'Big Data' katika mageuzi ya kiuchumi na maendeleo endelevu ya afrika," amesema Shekimweri.

Ameongeza kuwa NBS kwa kushirikiana na Ofisi za Takwimu za Afrika zitakuwa zinatekeleza lengo namba 17 la malengo endelevu ya Dunia ambalo linahimiza ushirikiano katika kutekeleza malengo hayo ambayo nchi za za Afrika zimeridhia utekelezaji wake.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa shughuli za kitakwimu NBS Emilian Karugendo amesema kuwa matumizi ya Takwimu rasmi ndio msingi wa kila kitu katika maisha,katika mipango na katika kufuatilia programu mbalimbali na utekelezaji wake.


"Kongamano hili ni kuelekea siku ya kilele cha maadhimisho haya ambapo siku moja kabla ya maadhimisho huwa wanafanya kongamano na kuwaweka pamoja watu tofauti tofauti kwa lengo a kuwa na mjadala wa kina unaolenga kujikita katika kaulimbiu hii na kuidadafua na kuona ni namna gani kama nchi wanaweza kuendana na kaulimbiu,"ameeleza.

Ameongeza kuwa moja ya mada ambazo zitajadiliaa ni matokeo ya sensa ya watu na makazi mwaka 2022 na mwongozo wa kitaifa wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 na matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 yanawezaje kutumika kwa pamoja na matokeo ya tafiti nyingine ili kuongeza matumizi na thamani ya Takwimu rasmi katika sekta ya kilimo nchini.

Kwa upande wake Mhadhiri Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika,Godfrey Saga ameeleza kuwa lengo kubwa la kongamano hilo ni kuweka ufahamu katika tasnia hiyo ya Takwimu kuanzia shughuli za ufundishaji masuala ya utafiti na masuala ya ushauri wa kitaalamu pamoja na kutumia taarifa hizo zinazotokana na takwimu mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI