Na Asha Mwakyonde,Dodoma
ZAIDI ya wanachuo 700 wa kada mbalimbali za Afya wanatarajiwa kuhitimu na kufanya mahafali ya saba katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi (DECOHAS), Disemba 15, mwaka huu sambamba na maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa kiongozi mkubwa kutoka serikalini.
Pia chuo hicho kinajivunia kuisaidia Serikali kutoa elimu ya afya ambapo zaidi ya tangu kuanzishwa kwake kimeshatoa wahitimu zaidi ya 4000 katika kada mbalimbali za afya.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma leo Novemba 15, chuoni hapo na Afisa Uhusiano wa DECOHAS,,Nicholaus Lwena amesema katika muongo huo mmoja chuo hicho kimejipambanua vyema kutoa elimu bora.
Lwena ameeleza kuwa mbali na kujipambanua wanahakikiaha watu wenye weledi wa hali ya juu katika fani zote zinazotolewa chuoni hapo.
Amefafanua kuwa chuo hicho kina wanachuo zaidi ya 3000 katika Kampasi zote mbili na wanachuo 4944 waliomaliza hapa tangu kuanzishwa kwake ambapo wengi wao wapo katika soko la ajira serikalini na sekta binafsi.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma,Utafiti na Uelekezi,Dk.George Adrianoamesema kuwa Wafanyakazi zaidi ya 400 wamepita katika Chuo cha DECOHAS na wengine zaidi ya 250 wanaendelea kuchapakazi.
"Tunawakaribisha kwenye sherehe hizi wafanyakazi waliokuwa hapa ambao kwa sasa wapo serikalini na katika taasisi, mashirika binafisi,"
amesema Dk.Adriano.
Katika sherehe hizo za miaka 10 na mahafali Msaani wa Kitaifa Rayvanny atakuwepo kutoa burudani.
0 Comments