MBUNGE MWAIFUNGA: RAIS DK.SAMIA ANASHUSHA FEDHA ZA MIRADI HAKUNA MAENEO YA KUJENGA


Asha Mwakyonde, Dodoma

MBUNGE wa Viti Maalum Hawa Mwaifunga (CHADEMA) ameeleza kuwa nchi inahitaji kupangiwa matumizi ya ardhi na kwamba kukiwa na matumizi bora ya ardhi watu hawatagusa eneo ambalo siyo lao hivyo endapo matumizi hayo ya ardhi hayatapangwa migogoro haitakwishwa.

Pia amesema Rais Samia Suluhu Hassan anashusha fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo, lakini unakuta hakuna maeneo ya kujenga kwa sababu kuna watu wanahodhi hayo.

Hayo ameyasema leo Februari  8,2024 Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala kuhusu utekelezaji wa shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii kwa mwaka 2023,Mwaifunga amesema mgogoro wa ardhi upewe kipaumbele ili kupunguza matatizo na changamoto za ardhi kwa wananchi.

Mbunge huyo amesema migogoro hiyo itazuka mingine kwa kuwa  serikali haijaamua kupanga matumizi bora ya ardhi,kila iitwapo kesho kutakuwa  na migogoro.

“Nimwambie tu Mheshimiwa Waziri (Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Slaa) hii migogoro anayokwenda kutatua leo,kesho itazuka,"amesema.

Mwaifunga ameeleza kuwa Mkoa wa Tabora una ardhi kubwa matajiri wachache wanakwenda kununua ardhi hiyo kwa ajili ya kuihodhi na baadaye wananze wauzia wengine huku akisema jambo hilo ni baya.

"Kama tungekuwa tumeshapanga matumizi bora ya ardhi kwenye maeneo yetu,tungejua hapa pangejenwa shule, hospitali, kituo cha afya, leo mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anashusha fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo, lakini unakuta hakuna maeneo ya kujenga kwa sababu kuna watu wanahodhi hayo

MALIASILI NA UTALII

Katika hatua nyingine Mbunge huyo ameonesha kukerwa na kitendo cha maeneo ya kihisitoria mkoani humo kutelekezwa.

“Tuna eneo moja la Taasisi pale Tabora lipo katikati ya mji,pale Luna sanamu ya mwalimu Nyerere ,katuka eneo hilo mwaka 1958 mwalimu Nyerere  alia machozi akiomba uhuru wa nchi hii.

Ameongeza kuwa eneo hilo ni changamoto halina umeme,majengo yamechakaa sanamu la Mwalimu Nyerere imechakaa watu wa Wizara ya Maliasi wana makumbusho, Malikale wanashindwa hata kututengenezea eneo ambalo mwalimu Nyerere alilia machozi wakati akiomba uhuru wa Taifa.

 “Mnashindwa kulifanya eneo hili kuwa la makumbusho,mnafanya nini  kwenye wizara,nimeongea kwa uchungu maana mnatuchosha mnaufanya Mkoa wetu unazidi kuwa mkongwe ,Mkoa wa Tabora umefunguka,tuwekeeni makumbusho ili vizazi na vizazi vijue Mkoa wetu umechangia katika uhuru wa Taifa hili,," ameeleza.

Aidha mbunge huyo ameipongeza  Mamlaka ya Wanyamapori (TAWA) ambao hivi sasa wameanza kutengeneza maeneo ya vivutio mkoani Tabora.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI