Na Asha Mwakyonde, Dodoma
BUNGE limepitisha bajeti ya Wizara ya Nishati ya shilingi trilioni 1.8 sawa na asilimia asilimia 95.28
kwa mwaka wa fedha 2024/ 2025, lengo likiwa ni kuwezesha Wizara hiyo kutekeleza mipango yake hasa ya kupeleka umeme kwa wananchi ambapo kukatika kwa umeme huo nchini kulichangiwa kwa kiasi kikubwa na upungufu wa umeme.
Akizungumza bungeni jijini Dodoma wakati akihitimisha bajeti ya Wizara ya Wizara ya Nishati,Waziri wa Wizara hiyo na Naibu Waziri Mkuu Dk. Doto Biteko
amewahakilishia wabunge na wananchi kuwa mgao wa umeme unaenda kumalizika na kwamba upungufu wa umeme huo ulikuwa ni megawati 410.
Naibu Waziri Mkuu huyo ameeeleza umeme unaouzalishwa ni kidogo kuliko mahitaji na kwamba uwezo wao wa kuzalisha umeme unakutana na mahitaji ambapo kunakuwa na mahitaji kidogo.
"Mheshimiwa Spika tukiwasha mitambo yetu yoye ya umeme hatuna mahali pengine pa kupeleka umeme,inabidi mitambo mingine tuisimamishe iwe 'standby ili kukitokea madhara au tatizo mahali fulani ,basi ule mtambo ambao upo kwa dharura unauwasha kwa ajili ya kuondoa hiyo changamoto ya umeme," ameeleza.
"Hivi leo ninavyozungumza mheshimiwa Spika tuna mitambo mbalimbali lakini mitambo ya Kinyerezi,mashine zote nne hatujaziwasha kwa sababu mahitaji ya umeme tunayoyahitaji nauwezo wa kuzalisha,uwezo wetu unakidhi amhitaji na kwa hiyo hakuna mgao,
"Sasa kuna jambo jingine umeme utakatika siyo kwa sababu ya upubgufu wa umeme bali ni kwa sababu nyinginezo ikiwemo miundombinu ,"amesema Dk.Biteko.
Amesema walichokieleza wabunge kuhusu kuchoka kwa miundonbinu ya umeme iliyopo sasa ,huku akikiri kwamba mashine nyingi za kuzalusha umeme zilizopo ntingi ni za muda mrefu tangu miaka ya 1970.
Pia amesema njia za kusafirisha umeme hadi zinfukie mteja nazo ni ndefu sana ambapo ikitokea shida mahali fulani watanzania wengi wanakosa umeme.
Ameongeza kuwa transfoma 87 zimeibwa na wapo waliokamatwa na kufikishwa mahakamani huku akisema mtu akichukua transfoma watu wengi watakosa umeme.
Pia amesema shida nyingine inatokea kipindi hiki cha mvua ambazo zineharibu miundombinu mbalimbali ikiwemo ya Tanesco huku akisema katika kuoindi hiki tu cha mvua nguzo 651 zimesombwa na maji.
Kufuatia hali hiyo Dk.Biteko amesema Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu.
"Tunafanya kila jitihada za kuhakikisha kwamba tunaimarisha miundombinu ya umeme ,ni kweli kwamba tunazo laini ndefu nchi hii tunahitaji vituo vya kupoza umeme 216 ,tulivyonavyo ni 131 ,tena navyo vingi vimechoka maana ni vya muda mrefu m," ameeleza.
Amesema kuwa wanahitaji kujenga vituo vipya 85 na vituo vingine vya kupozea umeme kwenye maeneo ambayo yapo nje ya grid 24 vinahitaji uwekezaji.
Awali Naibu Waziri wa Nishati,Judith Kapinga amesema Bajeti ya Wizara ya Nishati iliyoidhinishwa na Bunge ni shilingi 1,883,759,455,000 ambapo Shilingi 1,794,866,832,000 sawa na asilimia 95.28 ya Bajeti yote ya Wizara ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo na Shilingi 88,892,623,000 sawa na asilimia 4.72 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida.
Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa azma ya Serikali ni kuongeza kasi ya matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ikiwemo gesi na. kwamba lengo ni kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa nishati safi, salama, endelevu, yenye uhakika pamoja na kuondoa matumizi ya kuni na mkaa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Wabunge.
"Namshukuru Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya Nishati kupitia miradi mbalimbali kielelezo na maendeleo inayoendelea nchini" amesema Naibu Waziri Kapinga.
Amesema nyenzo muhimu ya kusaidia kutunza mazingira ni mkakati wa kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia umeshapitishwa na Baraza la Mawaziri na upo tayari kufanyiwa kazi.
0 Comments