Na Asha Mwakyonde, Dodoma
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), umesajili kampuni zaidi ya 50 katika maonesho ya Kitaifa ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane), ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Pia BRELA imetoa rai kwa Wafanyabiashara na Wakulima waweze kutembelea banda hilo kujionea mambo mengi mazuri ambayo Wakala huo wamewaandalia.
Akizungumza leo Agosti 6,2024 katika maonesho hayo Afisa Kumbukumbu kutoka BRELA Faridi Hoza wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao amesema kuwa wapo katika maonesho hayo kutoa huduma za usajili wa makampuni, usajili wa alama za biashara, usajili wa Ataza, leseni.
Aidha amesema kuwa wana toa huduma kwa watu mbalimbali huku akiwakaribisha Wakulima, Wafanyabiashara ili kuweza kufanya maombi ya usajili.
Aidha Mmoja wa wananchi waliotembela banda la Brela, Yahaya Hassan amewashauri watu wengi ambao wana changamoto ambazo zinahusu kampuni au majina ya kibiashara waweze kufika Katika banda hilo ili kupata huduma Huduma za papo kwa papo.
Hassan amesema kuwa kufika kwa kwake kwenye Banda hilo ni kufatilia taarifa za Kampuni ambapo ameishukuru kwa kuhudumiwa kwa wakati tofauti na angekwenda katika ofisi hizo baada ya maonesho.
0 Comments