WATU ZAIDI YA 1,000 WAMEPATIWA HUDUMA ZA UMIPAJI AFYA KWENYE MAONESHO YA WAKULIMA DODOMA

Na Asha Mwakyonde Dodoma 

WIZARA ya Afya inatoa bure huduma zinahusisha upimaji wa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, uchunguzi wa awali wa saratani ya mlango wa kizazi, saratani ya matiti, uzazi wa mpango pamoja na huduma za chanjo ya homa ya ini.

Huduma hizo zinatolewa katika maonesho ya wakulima na Wafugaji Nane nane ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma ambapo zaidi ya watu 1,000 wamepatiwa elimu ya masuala ya Afya.

Akizungumza leo Agosti 6, katika banda la Wizara hiyo kwenye maonesho hayo,Mratibu wa Mabadiliko ya Tabia katika Jamii kutoka Idara ya Kinga Wizara ya Afya, Grace Msemwa ameelezawanafanya uchunguzi na kutoa elimu kuhusu afya ya akili, huduma zote hizi zinatolewa bure kwahiyo tunawakaribisha wananchi wafike kwa wingi ili wawahudumie.

Mratibu huyo amesema kuwa wana dawati maalumu la uelimishaji masuala mbalimbali ya afya ambapo wanaelimisha kuhusu lishe, ugonjwa wa maralia, kifua kikuu na matumizi ya dawa asili

Post a Comment

0 Comments

ENDELEENI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA VIRUSI VYA UKIMWI” MHE. NDERIANANGA