MOI YATOA HUDUMA ZA KIBINGWA NANE NANE DODOMA, WANANCHI WAKARIBISHWA


Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

DAKTARI wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu Dk. Consolata Shayo kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI),amesema kuwa taasisi hiyo inatoa huduma za kibingwa kwenye maonesho ya wakulima na Wafugaji yanayofanyika Kitaifa viwanja vya nane nane Nzuguni jijini Dodoma ambapo imewapokea wagonjwa mbalimbali wakiwamo 
wenye matatizo ya lishe.

Dk. Shayo amesema wagonjwa wengine waliowapokea ni wale wenye matatizo ya mifupa, mgongo, kichwa, mishipa ya fahamu ambapo huduma hizo zinatolewa Bure katika banda la MOI.

Akizungumza leo Agosti 6,2024 katika maonesho hayo amesema kuwa mbali na lishe duni na wengine wana uzito mdogo kuliko urefu na wale wenye matatizo ya uchakavu wa migongo, mifupa na magoti.


Dk. Shayo ameongeza wengi wanaenda katika banda hilo kwa kuwa wana shida hiyo kutokana na umri wao na kwamba mwitikio wa wananchi ni mkubwa na wanaendelea kujitokeza kwa wingi.

Dk. Shayo amewashauri wananchi ambao bado hawajafika kwenye banda la MOI kuhakikisha wanafika ili waweze kusaidiwa kupatiwa huduma za kibingwa.

"kwa wale ambao wanahitaji matibabu zaidi tunawaandikia Rufaa ili waweze kwenda Hospitali kubwa na wengine wamekuwa wakiwaandikia dawa," ameongeza kuwa.

"Mfano kazi zetu tunazozifanya tunakaa mda mrefu bila kifanya mazoezi kukaa zaidi ya dakika 45 hadi lisaa bila kunyoosha miguu na mgongo kuna changia kuumwa mgongo pamoja na miguu, "amesema.

Amesema kuwa kutokana na aina ya maisha ambayo jamii imekuwa ikiishi hapo awali na ambavyo wanaendelea kuyaishi kwa sasa yanachangia kuleta madhara ya lishe.

Post a Comment

0 Comments

 MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI