BRITEN YAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA USHIRIKIANO MZURI NA MAREKANI, WAKULIMA ZAIDI YA LAKI 3 WAFADHILI NA USAID

Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

WAKULIMA waliofikiwa na mradi ambao unafadhiliwa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), ni zaidi ya 300,000 ambapo vijana na kwamba waliofikiwa na mradi huo 50,000 ambao wamepata ajira kupitia mnyororo wa thamani katika Sekta ya kilimo.

Akizungumza leo Agosti 8 katika maonesho ya wakulima na Wafugaji Nane nane ambayo yanafanyika Kitaifa viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma,

Mkurugenzi wa Shirika la Building Rural Incomes Through Entrepreneurship (BRITEN), Josephine Kaiza ameeleza kuwa vijana wengi wamepata ajira kwenye kilimo zikiwamo za kutoa huduma kwenye pembejeo na katika huduma za kidigitali.

Mkurugenzi huyo amelipongeza Shirika la Centro Internacional de Mejoramiento de MaĆ­z y Trigo (CIMMYT) kwa kuwaletea mradi ambao unafadhiliwa na USAID ambapo uwezesha kuwajengea uwezo wanawake na vijana nchini Tanzania.

"Katika maonesho haya tunaishukuru (CIMMYT), kwa kutoletea wa USAID pia tunaishukuru Shirikisho la Mageuzi ya Kijani Afrika (AGRA) kwa kuweza kutufadhili sisi mashirika haya ya nchi kuweza kuutekeleza huu mradi, amesema Kaiza.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa kwa sasa wanashukuru wameweza kujenga uwezo wa kina mama na kuleta ajira kwa vijana.

Aidha ameipongeza serikali kwa kuweza kuwasaidia mawazo kwenye mradi huo ambao wameweza kufuata shughuli za mradi wa ''Jenga Kesho Iliyobora'' maarufu kama (BBT).

Mkurugenzi huyo amempongeza Rais Dk Samia suluhu Hassan kwa jitihada za kuhakikisha kilimo kinawapatia ajira vijana na wanawake kwa kuruhusu wafadhili kufadhili miradi ya kilimo.

Awali Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk.Michael Battle alipotembelea mabanda mbalimbali ya bidhaa, Tasisi, Makampuni na Mashirika yanayofadhiliwa serikali ya Marekani USAID, amesema Marekani itaongeza Dola Milioni 20 katika kufadhili shuguli za Kilimo na miradi mbalimbali ya uzalishaji wa bidhaa na mazao kupitia mradi wa Feed The Future huku akisema ni fahari kwa Marekani kuwekeza zaidi nchini Tanzania lengo ni kuhakikisha kunakuwa na usalama wa chakula.

"Tanzania inanafasi nzuri ya kusaidia mataifa mengine kupata chakula cha uhakika ikiwemo Marekani, kuna mazao mengi yanayopelekwa marekani kutoka nchini humu mfano zao la kahawa" ameeleza.

Balozi Dk.Battle ameongeza kuwa kwa sasa zao Parachichi ambalo linavunwa kipindi cha mwaka mzima hapa Tanzania inasaidia Marekani kupata zao hilo kwa kipindi chote.

 

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU