ISLANDS OF PEACE TZ YASHUKURU KUFADHAILIWA NA USAID


Na Asha Mwakyonde Dodoma 

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Islands of Peace Tanzania limewamewafikia wakulima zaidi ya 3500 katika kuhamasisha na kughuhisha mifumo endelevu ya chakula kwa kutumia kilimo Ikolojia.

Pia Shirika hilo limefurahishwa kutembelewa na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk.Michael Battle pamoja na timu yake kuja kuona wakulima wao wanafanya nini kwenye suala zima la kutunza, kuhifadhi na kuendeleza mbegu zetu za asili.

Hayo yalisemwa leo Agosti 8,2024 na mkurugenzi wa Shirika hilo Asyesiga Buberwa mara baada ya kutelewa na Balozi huyo katika maonesho ya wakulima na Wafugaji Nane nane ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma amesema

 Shirika la Islands of Peace Tanzania linafanya kazi na wakulima wadogo wenye kumiliki ya ekari chini ya tatu waliopo vijijini ambao hata uwezo wa kununua pembejeo hawana.

Amesema kuwa wao ni wanufaika na ufadhil wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), na kwamba kazi yao kubwa ni kuhamasisha na kughuhisha mifumo endelevu ya chakula kwa kutumia kilimo Ikolojia.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa wanaendelea kuwahawasisha wakulima hao na kwamba wanafanya kazi na Shirikisho la Vyama vya Wakulima Wadogo Tanzania – (SHIWAKUTA), ambalo linawafikia wakulima zaidi ya 45,000 nchini.

Amesema kuwa Balozi Dk.Battle na timu yake wameona ni jinsi gani vijana wanaweza kujikita katika masuala ya kilimo kwenye maeneo zaidi ya kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao, kutengeza mbolea za asili kwa kutumia mbinu mbalimbali ambazo ni bunifu zinazowaletea kipato.


"Tunaishukuru serikali ya Marekani lakini pia omba na kueneza haya mashrikiano yaweze kuendeIea ili tuweze kuwafikia watu wengi zaidi hasa wakulima wadogo waliopo vijijini," amesema.

Ameongeza kuwa wanatamani kupanua wigo wa kazi zao wanazozifanya kwa kuwa wameona zinamanufaa kwenye suala la kuhifadhi mazingira kwenye kupata kipato cha Mwananchi na katka kuhakikisha ustawi wa wananchi hao inaboreka na unakua vizuri kwa sasa na kwa baadae.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa wao kama Shirika la Islands of Peace Tanzania wanafurahi kuwa miongoni mwa watu wanaofadhiliwa na shirika la USAID, huku akimshuru serikali ya Marekani kwa ufadhil wake

Alipotembelea mabanda mbalimbali ya bidhaa, Tasisi, Makampuni na Mashirika yanayofadhiliwa serikali ya Marekani USAID ambayo yameshiriki katika maonesho hayoBalozi wa Marekani nchini Tanzania Dk.Michael Battle amesema serikali ya Marekani inawekeza Mamilioni ya fedha za Kimarekani hapa nchini Tanzania na Marekani ndio mfadhili mkubwa wa shuguli za kimaendeleo.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU