TCRA YAWAKUMBUSHA WANANCHI KUWA MAKINI MATUMIZI YA SIMU, YAWATAKA KUTOKUFINGUA 'LINK'


Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),imewataka wananchi kuongeza umakini katika matumizi ya simu za mkononi na mtandao wa intaneti na kutofungua au kutosambaza viunganishi (links) wasivyovijua kwani vinaweza kuwaletea athari.

Pia Mamlaka hiyo imewataka wananchi kuendelea kuhakiki namba zao za simu na kwamba kwa suala hilo ni endelevu na kuripoti kwa watoa huduma namba wasizozifahamu ili ziweze kuondolewa.

Akizungumza leo Agosti 8,2024 na Waandishi wa habari kwenye Maonesho ya Wakulima na Wafugaji yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa TCRA, Rolf Kibaja,ameeleza baadhi ya watu wamekuwa si waaminifu wanaweza kutumia njia hiyo kupata taarifa ambazo zinaweza kuleta athari kwa muhusika.

Amesema wananchi hao wasipokee maelekezo yoyote kwa mtu anayejifanya akimwambia ni mtoa huduma bila kuhakikisha mtu ambaye anampigia na kumpa maelekezo.

Akizungumzia ushiriki wa katika maonesho hayo ili kuendelea kutoa elimu kwa umma, eneo ambalo watu wengi wamekuwa wakiuliza sana ni jinsi gani ya kuweza kujilinda, kuripoti kama wametapeliwa au kutoa taarifa.

Amesema uchumi wa kidigitali unatokana na umuhimu wa Mawasiliano ambapo kwao wakulima wanafanya mawasiliano pindi wanapo hitaji bidhaa za uzalishaji za kilimo na ufugaji.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA