TMA YAWAKUMBUSHA WANAOTUMIA VIFAA VYA HALI YA HEWA KUJISAJILI


Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imewataka ambao wana vifaa vya hali ya hewa kuhakikisha vifaa hivyo vimesajiliwa na Mamlaka hiyo TMA pamoja na kukidhi vigezo ambavyo vinahitaji Kitaifa wa nchi na kimataifa.

Pia wananchi wameshauriwa kuendelea kufatilia na kuzingatia sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa namba 2 ya Mwaka 2019 ambayo inatoa maelekezo mbalimbali kwa kila Mwananchi na kutumia hizo taarifa.

Hayo yamesemwa leo Agosti 8,2024 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ladislaus Chang'a wakati akizungumza navwaandishi wa habari kwenye banda lao lililopo katika maonesho ya kitaifa ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nanenane-Nzuguni jijini Dodoma

Ameeleza kuwa katika banda lao wapi wataalamu bingwa ambapo wameendelea kutoa hiyo elimu huku akisema Wakulima na Wafugaji wameendelea kutembelea na kutaka kupata taarifa ambazo wanaweza wakazitumia vizuri katika kuongeza tija na ufanisi kwenye shughuli zao za uzalishaji hasa kwenye kilimo.

 Dk. Chang'a ameongeza kuwa Dunia inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa, wananchi wote wanapaswa kufatilia kwa umakini taarifa za hali ya hewa za kila siku, mwezi, msimu ili kuweza kuongeza tija na ufanisi kwenye shughuli zao.

Akizungumzia maonesho hayo amesema kuwa katika maonesho hayo, wametembelewa na wanafunzi kutoka shule za Msingi, sekondari, vyuo mbalimbali, na wengi wao wakitaka kupata elimu zaidi ya hali ya hewa na mabadiliko yake.

"TMA inaendalea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya huduma za Hali ya Hewa pamoja na kuendelea kuwasisitiza wananchi na jamii kwa ujumla kuendelea kufatilia kwa makini na kuzingatia taarifa," ameeleza.

Ameongeza kuwa hivi karibuni watatoa taarifa za msimu wa Vuli ambapo wataweza kuwaeleza wananchi kwa kina nini matarajio yao katika msimu ujao wa Vuli.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU