Na Asha Mwakyonde, DODOMA
MKURUGENZI Mtendaji wa Mpango wa Kuendeleza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Geoffrey Kirenga amesema kuwa mpango SAGCOT unahudumia mazao 12 yakiwamo ya mboga mboga,soya, viazi, nyanya na chai.
Akizungumza leo Agosti 8,2024 mara baada ya Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk.Michael Battle kutembelea banda kubwa la wafanyabiashara wa zao la parachichi katika maonesho ya wakulima na Wafugaji Nane nane ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma
ameeleza kuwa katika muda wote ambao wanafanya nao kazi wakulima hao wamekuwa ni msaada mkubwa ambapo Nyanda za juu Kusini ndio kapu la chakula.
Mkurugenzi Mtendaji huyo ameeleza sehemu kubwa ya mafanikio yaliyopatikana Nyanda za juu Kusini sio uzalishaji bali hata katika suala la miundombinu ambapo ametolea mfano barabara ya Morogoro ambayo inaenda kwenye mto Kilombero ni maarufu kwa usalishaji wa sukari na miwa.
Amefafanua kuwa hiyo ni sehemu ya mafanikio ambayo Tanzania imeipata na wakulima kupitia wafadhili Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), na Ubalozi wa Marekani hapa nchini.
Kirenga ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia suluhu Hassan kwa jitihada za kufanya uwekezaji katika Sekta ya kilimo na nyinginezo.
"Jambo la muhimu ni kuendeIea kushirikiana kati ya nchi yetu na nchi ya Marekani lakini jambo la msingi ambalo ni muhimu sana sasa hivi ni kuendeleza biashara kati ya nchi yetu na Marekani," ameeleza Mkurugenzi Mtendaji Kirenga.
Kirenga amesema kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Michael Battle alivyopita katika banda la maparachichi ameweza kuongea na Sekta binafisi ambayo inauza matunda na inayoandaa utaratibu wa kupeleka matunda hayo nchini Marekani.
" Sasa hivi tumeanza kuuza zao la korosho katika soko la Marekani lakini pia Balaozi Dk.Battle ameweza kuongea na baadhi ya wafanyabiashara wanoongeza thamani mazao na mafuta ya parachichi hivyo mahusiano ya biashara ni muhimu kwa kuwa tunaendelea kuwasaidia wakulima wetu na wafanyabiashara," ameeleza na kuongeza kuwa:
Ni muhimu kwenye uwekezaji wa kibiashara huku akisema wafanyabiashara wa Marekani waje Tanzania na wafanyabiashara wa Tanzania waende Marekani kujifunza" amesema Kirenga.
Kwa mujibu wa Kirenga, Balozi wa Marekani nchini Dk.Battle amesema wanakiu ya kupata matunda ya parachichi na mengine kutoka nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla na kwamba hiyo ni fursa ya kuweza kupeleka bidhaa kwenye soko la Marekani.
Awali Balozi hiyo wa Marekani nchini Tanzania Dk.Battle alipotembelea mabanda mbalimbali ya bidhaa, Tasisi, Makampuni na Mashirika yanayofadhiliwa serikali ya Marekani USAID ambayo yameshiriki katika maonesho hayo ameahidi kuendelea kufadhili shuguli za kilimo, kuongeza dhamani ya bidhaa zitokanazo na mazao mbalimbali, kusafirisha bidha hizo na mazao ya Tanzania nchini Marekani sambamba na kufadhili shuguli zingine za uzalishaji maji na upatikanaji wa ajira.
0 Comments